MVOMERO
Na Mwandishi wetu
Club ya mpira ya wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe wameahidi kuchangia ujenzi wa vyoo na sehemu ya kubadilisha mavazi kwa Wasichana wa Shule ya Msingi Mzumbe, iliyopo wilayani Mvomero, mkoani Morogoro.
Hayo yalisemwa na Dk. Lucy Massoi, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Kimataifa, Baraza la Wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe, na kusema kwamba mkakati wa Chuo hicho ni kuendeleza mashirikiano na wahitimu wawe mabalozi wazuri kikitangaza Chuo.