Print this page

Pambano la Fury na Usyk lamkera promota

By February 09, 2024 639 0
TYSON FURY TYSON FURY

LONDON, Uingereza
Promota Frank Warren anasema kwamba Tyson Fury alikuwa akifanya mazoezi kama pepo, na ni ujinga kuhoji uhalali wa jeraha la jicho la Mwingereza huyo.
Fury mwenye uzito wa ‘heavyweight’, alipaswa kupigana na Oleksandr Usyk Februari 17 mwaka huu lakini akajiondoa kwenye shindano hilo baada ya kupata matokeo mabaya.
Pambano hilo lisilopingika la kuwania taji, limepangwa kufanyika tena Mei 18 mwaka huu nchini Saudi Arabia.
“Tyson anataka pambano. Kuna baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakitokea, sijawahi kusikia kitu kama hicho,” Warren alisema.
Fury ndiye bingwa wa WBC, huku Usyk wa Ukraine (37), akishikilia mataji ya WBA, WBO na IBF.
Pambano lao huko Riyadh linatazamiwa kuwa na bingwa wa kwanza wa uzito wa juu asiyepingika katika enzi ya mikanda minne.
“Sielewi jinsi watu hawa wanaishi nje ya mchezo huu,” Warren alisema juu ya wale wanaohoji kuhusu Fury.
Kuchanika kwa Fury juu ya jicho lake la kulia, kulihitaji matibabu ya haraka na kushonwa sana.
Hii ni mara ya tatu pambano la Usky na Fury liliahirishwa tangu mwaka 2023 na kuratibiwa upya kila mara.

Rate this item
(0 votes)
Japhet