DAR ES SALAAM
Bondia wa Masumbwi nchini, Hassan Mwakinyo amesema kuwa ujio wa pambano lake la ‘Usiku wa Utetezi wa Mkanda” ni sehemu ya kudhihirisha utemi wake kwenye mchezo huo.
Mwakinyo anautetea mkanda wake wa WBO Afrika aliouweka kama rehani ili kurudisha hadhi yake kwenye viwango vya ubora vya mchezo huo.
Pambano hilo litakalo fanyika Tarehe 16 Novemba 2024 katika ukumbi wa Werehouse Masaki Jijini Dar es Salaam, na litakuwa pambano ambalo litatoa taswira ya ubora wa bondia huyo kutoka hivi karibuni kuingia katika mvutano mkubwa na baadhi ya mabondia wenzake.
Hassan Mwakinyo amewaomba wadau na wapenzi wa mchezo wa ngumi kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuona ukubwa wake kwenye masuala ya ngumi.
“Maisha yangu siku zote mimi ni mapigano kutokana na dunia ninayoishi, hivyo hata mpinzani wangu atambua hilo kuwa sitamuacha salama kutokana na maandalizi niliyoyafanya”, alisema Mwakinyo.