VATICAN CITY, Vatican
Baba Mtakatifu Fransisko amekutana na Wanachama wa Chama cha Umoja wa Wasioona na wenye Ulemavu wa Macho (Vipofu) nchini Italia.
Pande hizo mbili zimekutana katika ukumbi wa Clementina, mjini Vatican, akiwaalika kutembea na kuwa Mahujaji wa Matumaini kama vile Pier Giorgio Frassati, Francis na Clara wa Assisi, au Teresa wa Mtoto Yesu.
Aliwahimiza kutambua kwamba kinachowategemeza katika juhudi zao ni lengo la mwisho, yaani ahadi ya kuwepo kwa upya ndani ya Yesu, ambaye hutoa furaha tofauti ambayo haibaki nje au juu ya uso.
Papa aliwatakia Wanachama hao heri ya Mwaka Mpya, akisema, “Uwe mwaka wa ukuaji wa kibinafsi, na pia katika urafiki kati yenu.”
Vile vile, aliwasihi kufikiri na kujichukulia kama ni watu wanaotembea, na walioko kwenye safari, na kwamba katika kila umri, watoto, vijana, watu wazima, wazee, daima wawe ni watu wa kusonga mbele bila kukata tamaa.