DAR ES SALAAM
Na Arone Mpanduka
Imepita miaka 21 sasa tangu kocha Jose Mourinho kupewa jina la utani la ‘Special One’, likiwa na tafsiri ya Mtu Maalum.
Jina hilo limekuwa kubwa duniani na hivyo kumtambulisha vilivyo katika medani ya soka.
Picha lilianzia mwaka 2004 ambapo Chelsea ilimtambulisha kwa waandishi wa habari kocha wao mpya, Jose Mourinho.
Raia huyo wa Ureno alijiunga na Chelsea akitoka kuwa bingwa wa Ulaya akiwa na FC Porto.
Waandishi wa habari wakamuuliza kama anaweza kurudia kufanya alichokifanya akiwa FC Porto, yaani kuahidi ubingwa na kuuchukua.