VATICAN CITY, Vatican
Wanajeshi na Polisi wametakiwa kutambua kwamba wameitwa na Mungu ili kutetea wanyonge, kulinda waamini, kuhamasisha watu kuishi kwa amani, pamoja na kuendeleza haki na amani kila mahali.
Hayo yalisemwa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni, Baba Mtakatifu Fransisko katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Vikosi vya Wanajeshi, Polisi na Usalama, aliyoiadhimisha mjini Roma hivi karibuni.
“Ni nani bora kuliko ninyi, wanajeshi na polisi wapendwa, wavulana na wasichana, wanaweza kushuhudia vurugu na kusambaratika kwa nguvu za uovu zilizopo ulimwenguni? Mnapigana nao kila siku. Kiukweli mmeitwa kutetea wanyonge, kulinda Waamini, kuhamasisha kuishi kwa amani kwa watu…
“Kila mmoja wenu anafaa kwa nafasi ya ulinzi, ambaye anatazama mbele sana, ili kuepusha hatari na kuendeleza haki na amani kila mahali. Ninawasalimu ninyi nyote kwa upendo mkuu, Ndugu wapendwa, ambao mmefika Roma kutoka sehemu nyingi za dunia kusherehekea Jubilei yenu maalum…..