Dar es Salaam
Na Laura Chrispin
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi amewasihi Waamini kutambua kwamba Bwana Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu aliyekubali kujinyenyekeza na kutoa mwili wake usulubiwe kwa ajili ya ukombozsi wa Wanadamu.
Askofu Ruwa’ichi alitoa wito huo hivi karibuni wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Siku ya Uwaka iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Clara-Mongo la Ndege Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.
“Imetimia siku 40 tangu kuzaliwa Yesu ambaye alijitoa sadaka kwa watu wake kwa sababu ya upendo aliokuwa nao kwa kuutoa mwili wake na kukaa kwetu, ikiwa ni hali ya unyenyekevu wa Kimungu, kwani mara zote ni mkamilifu kwa watu wake,”alisema Askofu Ruwa’ichi.