DAR ES SALAAM
Na Mathayo Kijazi
Waamini wamekumbushwa kuwalinda, kuwatunza, na kuwapenda Mapadri wao, na kamwe wasikubali Mapadri wao wachafuliwe na mtu mmoja au kikundi cha watu.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba alitoa wito huo hivi karibuni wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, alipofanya ziara yake ya kichungaji katika Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu – Buza, jijini Dar es Salaam.
“Sasa niwaombe kitu kimoja, endeleeni na ukarimu huo. Wapendeni Mapadri wenu, nafahamu kwamba mna Mapadri wawili hapa, jitahidini kuwapenda na kuwalinda, wetendeeni mema Mapadri wenu, msikubali Mapadri wenu wapate changamoto, msikubali Mapadri wenu wachafuliwe na mtu mmoja au kikundi cha watu, hakikisheni mnaendeleza ushirikiano kati yenu na Mapadri wenu katika Parokia hii ya Buza,” alisema Askofu Musomba.