Dodoma
Na Mwandishi wetu
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeshauri Serikali kusimamia vyema Mkandarasi anayejenga uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato jijini Dodoma ili akamilishe ujenzi huo kwa wakati.
Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso alisema kuwa ni vema mkandarasi akaharakisha ujenzi wa uwanja huo, ili kwenda na mkataba wa ujenzi.
Alifafanua kwamba kumekuwa na tabia kwa baadhi ya Wakandarasi kuomba kuongezewa muda wa ziada wanapopewa kazi, bila kujua muda utakapoongezwa na gharama nazo zinaongezeka.
Hivyo wao kama Kamati, wanashauri Serikali kwanza ni kumsimamia mkandarasi akamilishe ujenzi kwa wakati.
“Kumekuwa na tabia ya Wakandarasi wetu wanapopewa kazi wanaongeza muda wa ziada ambao hautakiwi uingezwa mara kwa mara, Hivyo tunaomba eneo hili Serikali isimamie, kwani anapoongezewa muda, na gharama zinazidi zaidi za ule mkataba uliokuwa umesainiwa,”alisema kiongozi.