Print this page

Wanandoa wapewa mbinu kufika mbali

By February 14, 2025 145 0
Wanajubilei Thomas Uiso na Misuka Makani wakirudia kiapo cha ndoa Takatifu mbele ya Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukrani kwa Mungu kwa Jubilei ya Miaka 25 kwa Wanandoa, iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mtakatifu Kizito – Kilongawima, jimboni humo. (Picha na Yohana Kasosi) Wanajubilei Thomas Uiso na Misuka Makani wakirudia kiapo cha ndoa Takatifu mbele ya Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukrani kwa Mungu kwa Jubilei ya Miaka 25 kwa Wanandoa, iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mtakatifu Kizito – Kilongawima, jimboni humo. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Wanandoa wametakiwa kupendana na kuvumiliana katika shida na raha siku zote za maisha yao, kwani katika maisha ya ndoa kuna mengi yanayotokea, hivyo bila kuvumiliana, ndoa hizo haziwezi kudumu.
Wito huo ulitolewa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukurani kwa Mungu kwa Jubilei ya Miaka 25 kwa Wanandoa jozi tatu ambao ni Thomas Uiso na Misuka Makani, Damas Mugashe na Rose Emanuel, Deusdedit Rutazaa na Jaove Ijumba, ilifanyika katika Parokia ya Mtakatifu Kizito – Kilongawima, jimboni humo.
“Ndoa ni uvumilivu, siyo mwezako akikukosea kidogo tu, wewe unakuwa na hasira muda huo huo, sio vizuri, lazima muwe watu wa kusameheana, kwa sababu ninyi mmekuwa mwili mmoja, lazima muwe watu wakulindana kwa makosa mnayokwazana,” alisema Askofu Musomba, na kuongeza;

Rate this item
(0 votes)
Japhet