Print this page

DEUS RWEGASIRA; Meneja Uzalishaji Maji Mstaafu anayetamba na Katoma Sound

Na Remigius Mmavele

Deusdedit Method Rwegasira almaarufu Mzee wa Katoma Band alizaliwa Aprili 26, 1963, Kata ya Katoma, mkoani Kagera, jirani kabisa na nyumbani kwa Askofu Mstaafu Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba. Baba yake alikuwa anaitwa Method Rwegasira ambaye alikuwa Mhandisi wa ndege katika Kikosi cha Anga, Ukonga jijini Dar es salaam na mama yake alikuwa Emiliana Alfred.
Alianza elimu ya shule ya msingi katika Shule ya Msingi Katoma A mwaka 1973, na baadae alihamia Shule ya Msingi Minazi Mirefu iliyopo jijini Dar es salaam, ambako alisoma kuanzia mwaka 1973 hadi 1979.
Mwaka 1983 alijiunga na Chuo cha Ufundi cha Dar es salaam katika Kozi ya GCE, na kuhitimu mwaka 1986, na kisha aliendelea na FTC kuanzia mwaka 1986, na kuhitimu mwaka 1989.
Mwaka 1990, alijiunga na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) katika Kambi ya Ruvu kwa mujibu wa Sheria, ambako alihitimu mwaka 1991. Mwaka 1992 aliajiriwa na Kampuni ya Uchukuzi ya Express Tanzania Limited, ambako alifanya kazi kwa mwaka mmoja akiwa fundi magari. Aliamua kuachana na kazi hiyo baada ya mwaka mmoja kwa ajili ya kutafuta maslahi mazuri zaidi.

Rate this item
(0 votes)
Japhet