Dar es Salaam
Na Laura Mwakalunde
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddeaus Ruwa’ichi amewataka Wanakwaya kutambua kwamba wanapoimba muziki Mtakatifu, wazo sio kutumbuiza bali ni kuinjilisha.
Rai hiyo aliitoa hivi karibuni katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Utume wa Kwaya Katoliki Tanzania (UKWAKATA), Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Petro-Oysterbay, jimboni humo.
“Wanakwaya siyo watumbuizaji na kama unataka kutumbuiza, basi ni vyema kwenda kwenye mahall ya disco… lakini ukitaka kuinjilisha kwa kuishi ukristo wako na katika kanisa lako, huku ukimshukuru Mungu kwa zawadi ya kipaji alichokujalia cha kuinjilisha kwa njia ya kuimba, salia Kanisani,”alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.
Aidha, alisema kuwa kila mbatizwa anaitwa kuwa shahidi wa Kristo kwa kutumia Kipaji alichojaliwa na Mungu, akiwaasa Wanaukwakata hao, kutumia vyema vipawa vyao.