Mwanza
Na Paul Mabuga
Maandishi yaliyoandikwa kwenye bajaji zetu, ambayo kwa muhtasari na kwa muktadha wa yaliyokusanywa katika makala haya, unaweza kusema ni kama kutoka, “Enzi za Mwalimu” hadi “Kwenye Ndoa Yenu...”:, na vilevile ni maneno yanayosema mengi yenye kusisimua, kuibua hisia, kufurahisha na hata kufikirisha, sembuse kutia hofu na kuogofya.
Ni kwamba licha ya barabara za miji yetu hapa nchini, kujaa watu na shamrashamra za kelele za honi, lakini pia zimesheheni falsafa ya Mswahili.. Sio kwenye vitabu au kwenye mikutano ya hadhara, bali kwenye mabango madogo yaliyobandikwa, au kuandikwa nyuma ya magari yetu ya usafiri, na vyombo vingine maarufu kama Bajaji.