Bagamoyo
Na Laura Mwakalunde
Askofu wa Jimbo la Bagamoyo, Mhashamu Stephano Musomba, amewataka Waamini kutokuwa na Roho dhaifu, za kushindwa kuvumilia shida na matatizo.
Askofu Musomba alisema hayo hivi karibuni, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Tatu ya Furaha ya Majilio, iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli-Bunju, jimboni humo.