DAR ES SALAAM
Na Mwandishi Wetu
Klabu ya soka ya Singida Black Stars, imesema kwamba ilishindwa kujizuia baada ya ofa nzito kutoka Simba SC, iliyomtaka kiungo mshambuliaji Clatous Chama.
Afisa Habari wa Singida, Hussein Massanza, alisema kuwa mwanzoni hawakuwa na nia ya kumuuza Chama, lakini uongozi wa Simba uliweka mezani pesa nyingi, ambazo ziliwafanya washindwe kumzuia Chama kurejea Msimbazi.