Print this page

USWAHILI: Kisawe cha Muongo, utambulisho, “Vibe” la Gen Z, na Shahada ya Berlin

Hayati Edwin Mtei Hayati Edwin Mtei

MWANZA

Na Paul Mabuga

Mjadala wa “Uswahili ni nini”, uliibuliwa hivi karibuni na mchambuzi Maggid Mjengwa, akirejea fikra za Jenerali Twaha Ulimwengu na marehemu Edwin Mtei. 
Swali hili limezua taharuki chanya: Je, Mswahili ni nani katika ulimwengu wa leo? Je, bado ni yule “muongo muongo” aliyemchukiza Mtei, au ni utambulisho uliopata sura mpya, kuanzia mitaa ya Dar es Salaam hadi jijini Berlin?
Jenerali Ulimwengu, akizungumza hivi karibuni, katika makiwa ya marehemu Edwin Mtei, alifungua ukurasa wa kumbukumbu uliosisimua wengi. 
Alieleza kuwa Mzee Mtei alikuwa na msimamo usioyumba, dhidi ya kile alichokiita “Uswahili.” Katika muktadha wa kujiuzulu kwake Uwaziri, Mtei aliamini kuwa mfumo wa “Uswahili”, ulikuwa kikwazo kwa uadilifu wa kitaifa.

Rate this item
(0 votes)
Japhet

Latest from Japhet