Pwani
Na Mwandishi Wetu
Kuelekea katika mbio za Boston Marathon, zitakazofanyika nchini Marekani mwezi Aprili mwaka huu, Mwanariadha Staff Sajenti Alphonce Simbu, amewaomba wadau wa michezo kumsapoti gharama mbalimbali za ushiriki.
Mwanariadha huyo alisema kwamba, sasa anaelekeza nguvu zake zote kwenye maandalizi ya Boston Marathon, huku akiwa na kumbukumbu nzuri ya kumaliza nafasi ya pili mwaka jana.