DAR ES SALAAM
Na Arone Mpanduka
Licha ya timu nne za Ligi Kuu kuwa nyuma ya ratiba, kutokana na ushiriki wa michuano ya kimataifa, uongozi wa Bodi ya Ligi umesema kuwa unasaka njia bora, ya kuhakikisha hakutakuwa na viporo vingi msimu huu.
Kwa sasa timu za Simba, Yanga, Azam FC na Singida Black Stars, zimeonekana kuwa na mechi chache zaidi za kucheza, ikilinganishwa na timu nyingine, kutokana na ushiriki wao wa kimataifa.