Print this page

Uvaaji viatu virefu unavyoathiri Wanawake kiafya

By February 13, 2026 14 0
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Beatrice Nangawe, akitoa elimu ya afya bora kwa wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi wa afya iliyofanyika hivi karibuni katika ofisi za MSD Kanda ya Mabibo jijini Dar es Salaam. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Beatrice Nangawe, akitoa elimu ya afya bora kwa wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi wa afya iliyofanyika hivi karibuni katika ofisi za MSD Kanda ya Mabibo jijini Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM

Na Edvesta Tarimo

Katika jamii nyingi, viatu vyenye kisigino kirefu vimejijengea nafasi ya kipekee kama alama ya urembo, hesima, hadhi na kujiamini kwa mwanamke. Kwa muda mrefu, kuvaa kiatu chenye kisigino kirefu kumechukuliwa kama sehemu ya mwonekano wa kitaaluma na kifahari, hususani katika mazingira ya kazi na hafla rasmi. Hata hivyo, nyuma ya mvuto huo wa nje, tafiti za kisayansi zinaendelea kuibua hoja nzito, kuhusu gharama ya kiafya inayoweza kujificha kwenye mtindo huu.
Kihistoria, kumbukumbu zinaonesha kuwa viatu vyenye kisigino havikuanza kama vazi la wanawake. Tafiti za kihistoria za mitindo zilizokusanywa na Fashion Institute of Technology, zinaonesha kuwa takribani mwaka 1000 BK, wanaume wa Uajemi waliokuwa wakipanda farasi, walitumia viatu vyenye kisigino, ili kuimarisha mshikamano wa mguu na farasi.

Rate this item
(0 votes)
Japhet

Latest from Japhet