Print this page

Majanga yachukua nafasi katika mahubiri Pasaka

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, akiongoza Adhimisho la Misa Takatifu ya Sikukuu ya Pasaka katika Parokia ya Bikira Maria wa Fatima-Msimbazi. Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, akiongoza Adhimisho la Misa Takatifu ya Sikukuu ya Pasaka katika Parokia ya Bikira Maria wa Fatima-Msimbazi.

Na Mwandishi wetu

Katika kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka mwaka huu, jamii imeonywa kuacha tabia ya kukimbilia kuchukua picha na video katika majanga, na kuanza kuzituma mitandaoni, badala yake waanze kutoa msaada kwa watu waliokumbwa na mkasa huo.
Onyo hilo lilitolewa hivi karibuni, na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, akiwataka watu wenye tabia ya kupiga picha na kuchukua video kwenye majanga, bila ya kutoa msaada, kuacha mara moja kufanya hivyo.

Rate this item
(0 votes)
Japhet