Print this page

Teknolojia yaipa ahueni Bodi ya Ligi

By September 11, 2026 12 0
Mwamuzi wa Kimataifa, Ahmed Arajiga akitazama marejeo ya picha kwenye video Support katika moja ya michezo ya Ligi Kuu ya NBC. Mwamuzi wa Kimataifa, Ahmed Arajiga akitazama marejeo ya picha kwenye video Support katika moja ya michezo ya Ligi Kuu ya NBC.

Dar es Salaam

Na Mwandishi wetu

Bodi ya Ligi Kuu imesema uwepo wa teknolojia mpya ya VS pamoja na mfumo wa kisasa wa kukata tiketi kwenye mechi za Ligi hiyo, umesaidia kupunguza malalamiko dhidi yao kutoka kwa mashabiki.
VS (Video Support) ni teknolojia mbadala ya video iliyoanza kutumika katika msimu huu ikichukua nafasi ya VAR (Video Assistant Referee) ambayo husaidia waamuzi kufanya mapitio ya matukio kadhaa yenye utata uwanjani.
Akizungumza hivi karibuni, Afisa Habari wa Bodi hiyo, Yahya Abushehe amesema mwenendo wa Ligi hiyo ni mzuri hasa katika raundi za kwanza za michezo yake.
Alisema msimu umeanza vizuri kwa maamuzi mengi kufanyika bila malalamiko katika mechi kadhaa zilizokuwa na matukio ya utata ambayo yaliamriwa na teknolojia hiyo ya VS.

Rate this item
(0 votes)
Japhet