MWANZA
Na Mwandishi wetu
Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba amezitaka Wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa, Taasisi na Mashirika ya Umma nchini, kuacha matumizi yasiyo ya lazima ili kuokoa fedha, zitakazoiwezesha Serikali kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo.
Dk. Mwigulu alitaja baadhi ya matumizi yasiyokuwa ya lazima, ikiwemo ununuzi wa magari mapya, wakati yaliyopo yanaweza kuendelea kutoa huduma, kuchapisha kalenda na kununua vifurushi vya zawadi.