Dar es Salaam
Na Nicolaus Kilowoko
Wakati kukiwa na uchunguzi wa vitendo vya upangaji wa matokeo, katika mashindano mbalimbali ya soka Tanzania Bara, huko visiwani Zanzibar, viongozi wa soka wameanza kuwashughulikia wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Katibu wa Mashindano ya Kombe la FA Zanzibar, Ali Bakari, alielezea namna timu zinavyojihusisha na upangaji wa matokeo, katika mashindano ya Kombe la Shirikisho, na kutolea mfano timu waliyoifungia ya Taifa Jang’ombe, kutokana na kupanga matokeo.