DAR ES SALAAM
Na Edvesta Tarimo
Afya ya akili ni moja ya vipengele muhimu zaidi vya ustawi wa binadamu, lakini mara nyingi hupewa nafasi ndogo katika mjadala wa afya.
Hata hivyo utafiti unaonesha kwamba, afya ya akili inajumuisha hali ya kiakili, kihisia na kijamii ya mtu, na ni msingi wa jinsi anavyokabiliana na changamoto za kila siku.
Licha ya kwamba kila mtu anapitia magumu maishani, kuna njia za kujikinga dhidi ya athari za majeraha ya kihisia (kiwewe), na kujenga uthabiti wa kukabiliana na hali ngumu.