Dar es Salaam
Na Pd. Richard Mjigwa- C.PP.S
Ilikuwa ni Novemba 8, mwaka 1984, Mtakatifu Yohane Paulo II (Papa), alipochapisha Waraka unaojulikana kama “Tot tantaeque” yaani “Bikira Maria ameidhinishwa kuwa Mlinzi na Mwombezi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, Sherehe inayoadhimishwa kitaifa kila mwaka ifikapo Desemba 9.
Katika mkesha wa uhuru wa Tanganyika, Mtakatifu Yohane XXIII, alitunga Sala Maalumu kwa ajili ya kuiombea Tanganyika, ili uhuru wake uweze kuwanufaisha watu wake.