DAR ES SALAAM
Na Remigius Mmavele
Papy Tex mwimbaji mwenye sauti ya kuvutia na ya kipekee jina lake lake halisi ni Matolu Dode Jean , alizaliwa Juni 28, 1952 katika jiji la Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Baba yake mzazi alikuwa ni raia wa nchi ya Angola na mama yake kutoka Kongo ya Kati, alilelewa na Joséphine Matolu. Ni mwanamuziki maarufu duniani, mwandishi , mtunzi na mtayarishi wa muziki ambaye sauti yake ya huzuni na nyimbo zake zimeacha alama katika fikra za watu na bado zinaacha kumbukumbu zisizofutika katika kumbukumbu ya pamoja.