Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Serikali yawatengea bil. 48/- Wanafunzi wa Stashahada

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (kulia) akiweka Jiwe la Msingi la Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya (CUCOM) wakati wa sherehe za ufunguzi wa chuo hicho. Kushoto ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Mhashamu Gervas Nyaisonga na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (kulia) akiweka Jiwe la Msingi la Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya (CUCOM) wakati wa sherehe za ufunguzi wa chuo hicho. Kushoto ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Mhashamu Gervas Nyaisonga na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MBEYA

Na Hassan Shayo

Serikali imesema kuwa imetenga jumla ya Shilingi bilioni 48/-, kwa ajili ya mikopo ya Wanafunzi wa Stashahada katika mwaka wa masomo wa 2023/2024.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema hayo katika sherehe za ufunguzi wa Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya (CUCOM), zilizofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho.
Alisema kuwa mpango huo ambao ni maono na maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan unalenga kuhakikisha elimu inayotolewa inakuwa bora na kuwezesha wahitimu wa vyuo nchini kujiamini na kumudu ushindani wa kitaifa na kimataifa.
“Lengo jingine la Mheshimiwa Rais Dk. Samia ni kuona vijana wengi wanapata elimu itakayowapa ujuzi na uwezo wa kushiriki katika ujenzi wa Taifa,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa alisema Serikali imetenga Dola za Kimarekani milioni moja kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), ambazo zinasomesha Wahadhiri 27 kutoka Vyuo Vikuu visivyo vya Serikali.
Waziri Mkuu aliongeza kuwa fedha hizo pia zitatumika kugharamia wahadhiri saba katika ngazi ya Shahada ya Umahiri na 20 katika Shahada ya Uzamivu kwa programu za afya na sayansi shirikishi.
“Kupitia mradi huu Serikali imekuwa ikivifikia vyuo vikuu binafsi. Kitendo hicho kinaonesha dhamira ya dhati ya Serikali yetu ya kuiwezesha sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu kwa ngazi zote.
“Hii ni kutokana na ukweli kwamba Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na sekta binafsi katika utaoaji wa elimu kuanzia ngazi ya awali hadi elimu ya juu,”alisema Majaliwa.
Kwa mujibu wa Majaliwa vyuo vinavyomilikiwa na taasisi zisizo za Serikali vinatakiwa kuweka mpango mkakati wa kuongeza idadi ya wanataaluma hususan maprofesa, wahadhiri waandamizi na wahadhiri kwa maeneo ya programu zinazotolewa.
Katika hatua nyingine, Majaliwa alisema kuwa Serikali inathamini na kutambua mchango wa madhehebu ya dini, ikiwemo Kanisa Katoliki kwa kuwa mstari wa mbele katika utoaji wa huduma kwenye sekta mbalimbali, ikiwemo za afya, elimu na ustawi wa jamii.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Chuo hicho, Askofu John Ndimbo, ameishukuru Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (Tanzania Commision for Universities: TCU) kwa kuona umuhimu wa kukipa chuo hicho hadhi ya Chuo Kikuu, baada ya kutimiza masharti yote.
“Kupitia tume maalum iliyoundwa na Tume ya Vyuo Vikuu, ilijiridhisha na uboreshaji wa miundombinu, ndipo tulipewa hadhi ya chuo kikuu, TCU imekuwa mlezi bora kwetu.”
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Franklin Rwezimula ambaye amemuwakilisha Waziri wa Elimu kwenye ufunguzi huo, amelipongeza Kanisa Katoliki kwa namna linavyowekeza kwenye sekta ya elimu.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.