Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Serikali kushirikiana na Jumuiya wasioona

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Hemed Suleiman Abdulla (kulia) akizunguza na baadhi ya maafisa wa Serikali baada ya kuahirisha Maadhimisho ya Kuongeza Uwelewa kwa Jamii Juu ya Watu Wenye Ulemavu yaliyofanyika Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Mkoa wa Kaskazini Unguja. Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Hemed Suleiman Abdulla (kulia) akizunguza na baadhi ya maafisa wa Serikali baada ya kuahirisha Maadhimisho ya Kuongeza Uwelewa kwa Jamii Juu ya Watu Wenye Ulemavu yaliyofanyika Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, itaendelea kushirikiana na Jumuiya ya Wasioona Zanzibar (ZANAB), na Jumuiya nyingine za watu wenye ulemavu, ili kuweka mazingira wezeshi yatakayowasaidia watu wenye ulemavu kufaidika na fursa mbalimbali nchini.
Rais Mwinyi aliyasema hayo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla wakati wa kuahirisha Maadhimisho ya Kuongeza Uwelewa kwa Jamii Juu ya Watu Wenye Ulemavu katika viwanja vya mpira wa Mto wa Pwani Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema kwamba kwa kutambua kuwa watu wenye ulemavu wamekuwa wakikumbana na chamgamoto mbali mbali katika jamii, kumeanzishwa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu na Mabaraza ya Wilaya ya watu wenye Ulemavu yenye dhamana ya kusimamia, kutekeleza, kutetea na kulinda haki na fursa za watu wenye Ulemavu.
Rais Dk. Mwinyi alisema Serikali imetoa nafasi za Uongozi kwa watu wenye ulemavu katika Wizara mbalimbali, ambapo wamekuwa wakitekeleza majukumu kwa ufanisi mkubwa, jambo linalotoa hamasa kwa Serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa wenye ulemavu.
Dkt. Mwinyi alisema Serikali itahakikisha Sheria ya Watu Wenye Ulemavu inafanyiwa kazi na kupelekwa Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kujadiliwa, na hatimaye kupitishwa kuwa Sheria kamili, ikitoa miongozo kwa Taasisi na Jumuiya za watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kufanikisha malengo yao waliyojipangia.
Alibainisha kuwa kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, Serikali imekuwa ikichukua hatua za kuweka mazingira bora kwa watu wenye ulemavu, ikiwemo kutunga Sheria ya watu wenye Ulemavu Namba (8) ya Mwaka 2022 kwa lengo la kulinda na kutetea haki na fursa za watu wenye ulemavu.
Aidha, Rais Mwinyi alisema Serikali kupitia Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, itaandaa programu maalum itakayowajengea uwelewa wananchi juu ya kutambua haki na wajibu wa watu wenye ulemavu katika Mikoa yote ya Zanzibar.
Sanjari na hilo, Rais Dk. Mwinyi alitoa wito kwa Jumuiya za Watu Wenye Ulemavu kuongeza nguvu zaid ya uwajibikaji, na kuwahamasisha watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa mbali mbali zinazojitokeza katika Taifa.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Dk. Khalid Salum Muhammed alisema, Serikali zote mbili zimefanya mapitio ya Sera na Sheria kuhakikisha watu wote wanapata haki sawa, ikiwa ni pamoja na makundi maalum katika nyanja zote za kiuchumi na kijamii.
Dk. Khalid alifahamisha kuwa Serikali kupitia Mfuko wa Uwezeshaji, imejipanga kumaliza kilio cha muda mrefu cha watu wenye ulemavu kwa kuwapatia mikopo itakayowasaidia kujiendeleza kiuchumi katika miradi yao, pamoja na kujikimu kimaisha.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.