Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Rais Yanga kulipwa mamilioni CAF

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Rais wa Klabu ya soka ya Yanga, Injinia Hersi Said huenda akaanza kulipwa mamilioni yatokanayo na posho ya mwaka kupitia nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama cha Vilabu Afrika.
Shirikisho la soka Afrika CAF linapendekeza posho ya kila mwaka ya dola 50,000 za Kimarekani kwa Mwenyekiti wa Chama kipya cha Vilabu vya Afrika, ikiwa ni ajenda ya Mkutano Mkuu wa 46 wa Kawaida wa CAF utakaofanyika nchini Ethiopia Oktoba 22 mwaka huu.
Kiasi hicho atakachopata Hersi kwa mwaka kwa pesa za Kitanzania ni shilingi milioni mia moja thelathini na sita na laki tano (136,500,000).
Uwezekano wa kupata kiasi hicho cha posho ni pale wajumbe wa Mkutano huo watakaporidhia kwa pamoja pendekezo la ajenda hiyo.
Ikumbukwe kuwa Desemba mosi mwaka jana, Hersi alishinda nafasi hiyo ya kuongoza Chama cha Vilabu Afrika.
Siku chache baadaye ndani ya mwezi huo huo, CAF ilimteua Hersi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi za Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) na Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN).
Hersi aliteuliwa kuingia katika Kamati hiyo kwa vile ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, nafasi aliyoipata baada ya kuukwaa uongozi wa Chama cha Vilabu Afrika.
Hersi aliingia madarakani Yanga akirithi mikoba ya Dk. Mshindo Msolla, ambapo katika uongozi wake amefanikiwa kuibadilisha timu hiyo kucheza soka la kisasa, huku ikifanikiwa kusajili wachezaji wenye viwango vya juu Afrika.
Timu hiyo msimu huu imefanikiwa kupenya na kuingia katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika sawa na msimu uliopita, ambapo ilifanikiwa kufika katika hatua ya makundi na kuishia robo fainali, na baadaye kutolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Mwaka juzi Yanga ilicheza fainali za Kombe la Shirikisho barani Afrika na kufungwa na USM Algier katika mchezo wa fainali.
Septemba 16 mwaka huu, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) (EXCO) ilitangaza kuwa Mkutano Mkuu wa 46 wa Kawaida wa CAF utafanyika Addis Ababa, Ethiopia mwezi Oktoba.
Awali, mji wa Kinshasa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ulichaguliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa 46 wa Kawaida, lakini kutokana na sababu ambazo hazijawekwa wazi, DRC ilisema haiwezi kuandaa hafla hiyo.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.