Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Chansela wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Malawi ahimiza uadilifu

Chansela wa Chuo Kikuu cha Katoliki cha Malawi, Askofu Martin Anwel Mtumbuka. Chansela wa Chuo Kikuu cha Katoliki cha Malawi, Askofu Martin Anwel Mtumbuka.

LILONGWE, Malawi

Chansela wa Chuo Kikuu cha Katoliki cha Malawi, Askofu Martin Anwel Mtumbuka, ametoa mwito wa kuanzishwa kwa wahitimu, wanaozingatia uadilifu na maadili thabiti, pamoja na ubora wa kitaaluma.
Akizungumza wakati wa Mkutano wa 25 wa Chuo Kikuu, kwa ajili ya utoaji wa Astashahada, Stashahada na Shahada, uliofanyika Ijumaa iliyopita, Askofu Mtumbuka alieleza wasiwasi wake, kuhusu idadi inayoongezeka ya watu walioelimika, ambao hawana uadilifu katika majukumu yao ya kitaaluma na utumishi wa umma.
“Tayari tuna watu wa kutosha walioelimika, lakini kwa kusikitisha, tuna watu wengi sana waliopotoka. Tunachohitaji sasa ni wanaume na wanawake walioelimika, ambao watahudumu kwa uaminifu, uadilifu na huruma,” alisema Askofu Mtumbuka.
Msemaji wa kuanza kwa Sherehe hiyo, Mheshimiwa Jaji Annabel Mtalimanja, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC), pia aliwasihi wanafunzi waliohitimu hivi karibuni, kukataa ufisadi na rushwa, akielezea kuwa ni vikwazo vikubwa kwa maendeleo ya taifa.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.