Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Kitenge cha wajane, wagane chazinduliwa

Mkurugenzi wa Utume wa Walei Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Vitalis Kasembo, akizindua kitenge cha Wajane na Wagane katika Ofisi za Halmashauri ya Walei zilizopo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, jimboni humo. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho cha Kitume, Sweetbetha Mzungu. (Picha na Mathayo Kijazi) Mkurugenzi wa Utume wa Walei Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Vitalis Kasembo, akizindua kitenge cha Wajane na Wagane katika Ofisi za Halmashauri ya Walei zilizopo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, jimboni humo. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho cha Kitume, Sweetbetha Mzungu. (Picha na Mathayo Kijazi)

Dar es Salaam

Na Mathayo Kijazi

Mkurugenzi wa Utume wa Walei Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Vitalis James Kassembo amezindua kitenge cha Chama cha Kitume cha Wajane na Wagane, akiwataka kuutumia vema mradi huo katika kuendeleza utume kupitia chama chao.
Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni katika ofisi ya Halmashauri ya Walei iliyopo katika  viunga vya Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, jimboni humo.
Padri Kassembo aliwaasa wote watakaonunua kitenge hicho kuwa waaminifu, akisema kwamba anayechukua vitenge vya idadi fulani, arudishe fedha inayolingana na idadi ya vitenge hivyo.
“Mradi huu utusaidie pia kuendeleza utume. Lakini pia kama wanautume kuweza kujitawala vizuri sisi kama wanachama wa chama hiki. Maana yake tunaongea kuhusu uaminifu katika yale ambayo tutakuwa tumekabidhiwa, kama umekabidhiwa vitenge kumi, basi urudishe fedha ya vitenge kumi, usilete kona kona, kwa sababu ukileta kona kona, tunakwama wote,” alisema Padri Kassembo.
Aliwasisitiza kuutumia mradi huo kuwaunganisha na kuwafanya wawe wamoja zaidi, akiwaasa kutotengana kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo za kutokuwa waaminifu.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.