Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Waimarishwa waitwa kuishuhudia Injili

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, OFMCap akitoa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kwa mmoja wa vijana wa Parokia ya Mtakatifu Nicholaus wa Tolentino - Msingwa, jimboni humo wakati wa adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti hiyo. Kushoto ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Geofrey Mtitu -OSA. Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, OFMCap akitoa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kwa mmoja wa vijana wa Parokia ya Mtakatifu Nicholaus wa Tolentino - Msingwa, jimboni humo wakati wa adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti hiyo. Kushoto ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Geofrey Mtitu -OSA.

Na Mathayo Kijazi

Imeelezwa kuwa vijana wakishapokea Sakramenti ya Kipaimara, hawawi watoto tena, bali wanakuwa Wakristo wakomavu, na wenye kuwajibika katika kuishuhudia Injili ya Yesu Kristo.
Hayo yalisemwa hivi karibuni, na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi - OFMCap, wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara, katika Parokia ya Mtakatifu Nicholaus wa Tolentino - Msingwa, jimboni humo.
“Kama kwenye Ubatizo walizaliwa, kwenye Kipaimara wanakamilishwa, wanafanywa kuwa Manabii, wanakabidhiwa Utume, wanapewa jukumu la kuishuhudia Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo;
“Kwa hiyo vijana wapendwa, wanangu wapendwa, leo mnaanza ngwe mpya, ngwe mpya ya safari yenu ya imani. Kuanzia leo mkiwa mnarudi nyumbani, mkiwa mmepata Kipaimara, jitambueni kuwa ninyi sio watoto tena, utoto mtaucha pale kwenye mlango wa Kanisa. Na Paroko naomba kuanzia leo usiwaite tena watoto, waite Waimarishwa, waite watu wakomavu, waite watu wenye kuwajibika,” alisema Askofu huyo.
Aidha, Askofu Mkuu aliwasihi vijana hao kutokumhadaa Kristo, na kwamba wamshuhudie kwa maneno, matendo na kwa maisha yao yote.
Sambamba na hayo, aliwasisitiza kutoona aibu kusema mbele za watu kwamba, wanamuungama Kristo katika maisha yao, kwani kazi kubwa wanayotumwa kuifanya, ni kuitetea imani yao.
“Nanyi vijana wapendwa, hakikisheni kwamba hamumhadai Kristo, bali mnamshuhudia kwa maneno, kwa matendo, na maisha yenu yote. Na msione haya kujibainisha kuwa Wakristo, msione haya kusema kwamba, ‘Mimi namuungama Kristo Mwokozi wangu aliyeteswa, aliyekufa na aliyefufuka’. Simameni imara, simameni kidete kuujenga Ufalme wa Kristo,” alisema Askofu huyo.
Wakati huo huo, Askofu Mkuu Ruwa’ichi alitoa wito kwa wazazi, kushirikiana na watoto wao, katika kuuendeleza utume huo unaowapasa.
Pia, aliwasihi Mapadri, Makatekista pamoja na Viongozi wa Kamati Tendaji, kuhakikisha kuwa wanashikamana na kusindikizana na vijana hao, katika safari ya kuujenga Ufalme wa Mungu.
Kwa upande wake Paroko wa Parokia hiyo ya Msingwa, Padri Geofrey Mtitu - OSA, alimshukuru Askofu Mkuu Ruwa’ichi, kwa kufika parokiani hapo, na kuadhimisha Misa hiyo Takatifu.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.