Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Makonda apigia debe uwanja wa AFCON

ARUSHA

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema kuwa ajira za ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu ambao unatarajiwa kutumika katika mashindano ya Mataifa ya Afrika (African Cup of Nations: AFCON) mwaka 2027, zinapaswa kuwalenga zaidi Watanzania, badala ya wageni.
Akizungumzia kuhusu umuhimu wa mradi huo, Makonda alisema kuwa ujenzi wa uwanja huo umeleta nafuu ya maisha kwa wakaazi wa Mkoa huo ambao kwa kiasi kikubwa watapata kipato kutokana na kazi ya ujenzi.
Makonda (pichani) pia aliagiza kuwa shughuli zote zinazoendelea katika ujenzi wa uwanja huo, wahusika wakuu wawe ni Watanzania, huku akisistiza ununuzi wa malighafi zozote za ujenzi uzingatiwe ndani ya Mkoa wa Arusha.
Alisema kuwa kutokana na kusaini kwa Mkataba wa ujenzi huo kati ya Serikali na wahandisi wa ujenzi wa ujanja kumeongeza thamani katika maisha ya watu mbalimbali wa Arusha, huku akitamani kuona watu wa maeneo hayo wanakuwa wa kwanza katika kuangaliwa kwenye kupata ajira.
Kwa upande mwingine alisisitiza umakini uzingatiwe katika kujenga uwanja huo, kwani utafanyiwa uchunguzi na wataalamu mbalimbali lakini pia kujengwa katika viwango kutasaidia kuitangaza Serikali ya Awamu ya Sita kuwa makini katika miradi yake.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.