Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Pawasa ‘aing’ata sikio’ Simba

Biniface Pawasa Biniface Pawasa

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Beki wa zamani wa timu ya soka ya Simba, Boniface Pawasa ameushauri uongozi wa klabu ya Simba kuhakikisha unafanya maboresho ya kikosi ili iweze kurejesha ufalme wake katika msimu ujao wa 2024/25.
Simba imemaliza msimu uliopita ikiwa haina mafanikio kwenye malengo iliyojiwekea baada ya kuambulia Ngao ya Jamii pekee, huku ikikosa taji la Ligi Kuu na la Shirikisho la soka nchini TFF.
Akizungumza kuhusiana na kitu ambacho timu hiyo inapaswa kufanya, Pawasa ambaye aliwahi kuichezea Simba kwanzia mwaka 2001 hadi 2005 alisema kuwa wanapaswa kusajili wachezaji wapya wa kitaifa na kimataifa ili kusalia kwenye soko la ushindani.
Alisema kuwa msimu uliopita Simba ilisajili kwa kubahatisha, kitu ambacho kwenye soka la sasa hakifanywi na timu nyingi ambazo zina malengo makubwa ya kufika mbali.
“Mimi ukiniuliza kwa wachezaji wa kimataifa nani anapaswa kubaki nitakwambia wabaki watu watatu tu, beki Che Malone, Babacar Sarr na mshambuliaji Freddy Michael Kouablan. Hao wengine ni wa kawaida sana, hawanishawishi kuendelea kuvaa jezi ya Simba” alisema Pawasa.
Aliongeza kuwa wachezaji hao wanapaswa kuongezewa wengine wenye viwango bora zaidi ili waweze kuwasaidia kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa.
Pia, alibainisha kwamba kilichoigharimu Simba msimu uliopita ni kuwa na wachezaji wengi wasiojituma na wenye nidhamu mbovu, huku kila mmoja akijiona mkubwa kuliko klabu.
Pawasa ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Soka la Ufukweni, alienda mbali zaidi kwa kuiangalia timu ya Taifa Stars akisema kwamba wekundu hao wanapaswa kufanya usajili kwa maslahi ya timu ya taifa.
“Zamani timu hizi zilikuwa zinasajili wachezaji wazuri wazawa ambao ninaamini wapo, na faida kubwa inakuja kupatikana kwenye uteuzi wa kikosi cha timu ya taifa. Siku hizi tunajaza wachezaji wengi wa kimataifa, linapokuja suala la timu ya taifa tunanza kuhangaika, hasa jinsi gani ya kupata washambuliaji na mabeki,” alisema.
Alisema kuwa klabu za Tanzania zimekuwa zikifanya vizuri katika misimu ya sasa kwa msaada mkubwa wa wachezaji wa kigeni, kitu ambacho kinampa hofu kubwa.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.