Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Wasimamizi wakumbushwa kutimiza wajibu

Waamini wa Parokia ya Mtakatifu Clara-Magole, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakiwa kanisani wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara. (Picha na Yohana Kasosi) Waamini wa Parokia ya Mtakatifu Clara-Magole, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakiwa kanisani wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, amewaasa Wasimamizi wa vijana wa Sakramenti ya Kipaimara kuhakikisha wanawalea vijana wao kwa kuwaimarisha kiimani.
Askofu Mchamungu alitoa wito huo katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara, iliyofanyika Parokia ya Mtakatifu Clara_Magole, jijini Dar es Salaam.
Askofu Mchamungu alisema kwamba wasimamizi wengi hawajui majukumu yao, japokuwa wanasimamia watoto na kuacha kutimiza wajibu wao.
“Wakifanya sherehe na kula pilau basi hawana muda tena na huyo kijana aliyemsimamia, ndugu zangu wasimamizi mnaosimamia iwe Ubatizo, Kipaimara,  na waomba sana majukumu yenu mhakikishe mnayatimiza,”alisema Askofu Mchamungu.
Aidha, aliwasihi vijana hao kutoacha kwenda kanisani, kwani kufanya hivyo, watayumbishwa kiimani.
“Msiache kuja kusali, muwe watu wa sala kila muda… lakini pia ndugu zangu waamini, nanyi msije mkadanganywa na manabii wasio na Imani Takatifu Simameni imara siku zote,”aliongeza kusema Askofu Mchamungu.
 Askofu Mchamungu aliwaomba watu wenye ndoa kuhakikisha wanaiishi Sakramenti yao vizuri, bila kuwa na vikwazo vya mivurugano katika ndoa zao.
Askofu Mchamungu aliwapongeza Waamini kwa kupanda hadhi na kuwa Parokia kamili, akiwasihi kuungana ili Parokia yao isonge mbele.
Kwa upande wake Paroko wa Parokia hiyo, Padri Singano, alimshukuru Askofu Mchamungu kwa kuwapatia vijana Sakramenti ya Kipaimara.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.