Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Watawa wafundwa unyenyekevu

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba (mwenye fimbo ya Kichungaji), akiwa katika maandamano ya kutoka kanisani baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei. Kushoto ni Askofu Msaidizi wa Jimbo hilo, Mhashamu Henry Mchamungu. (Picha na Yohana Kasosi) Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba (mwenye fimbo ya Kichungaji), akiwa katika maandamano ya kutoka kanisani baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei. Kushoto ni Askofu Msaidizi wa Jimbo hilo, Mhashamu Henry Mchamungu. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba amewataka Waamini kuwa wanyenyekevu, kwani utawasaidia kuuona ukuu wa Mungu.
Askofu Musomba alisema hayo wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 25 na 50 ya Upadri, iliyoadhimishwa katika viwanja vya Kituo cha Msimbazi, jimboni Dar es Salaam.
“Katika hilo ni kwamba sifa zimwendee Mungu kwa makuu aliyowatendea ndugu zetu Wajubilanti kwa miaka 25 na miaka 50. Si rahisi hivyo, na ndiyo maana haya yote yanahitaji sana unyenyekevu. Katika unyenyekevu, ndipo tunapotambua ukuu huu wa Mungu katika maisha yetu,” alisema Askofu Musomba.
Musomba aliwaasa Wakristo kumshukuru Mungu kwa zawadi ya Makuhani, akiwasihi kutambua kwamba Makuhani hao ni Kristu mwingine.
“Tunapoadhimisha haya yote, tunathamini sana wito huu mkubwa wa Ukuhani. Kwa maneno mengine hawa Makuhani ambao ni Yesu mwingine. Na katika kumshukuru huyu Kristo, tumshukuru Mungu tumeona makuu anayotutendea kwenye maisha yetu. Na katika kuyaona hayo makuu, siyo kwamba tunajivunia kwamba tumeweza, ila tunamshukuru Mungu, na tunamsifu yeye peke yake,” alisema Askofu huyo.
Sambamba na hayo, alikumbusha kile kilichoendelea katika Kongamano la 5 la Kitaifa la Ekaristi Takatifu juu ya Ukuu wa Adhimisho la Misa Takatifu, na kwamba wanaojongea mbele za Mungu, Mungu hawezi kuwaacha.
Wakati huo huo, Askofu Musomba aliwapongeza Mapadri hao kwa Jubilei yao ya Miaka 25 na 50 ya Upadri, akisema kwamba wamefanya kazi kubwa kwa kuweza kukaa katika utume wao, pamoja na kudumisha utambulisho wao kama Makuhani.
Askofu huyo aliongeza kwamba kama Wanajimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wameziona kazi pamoja na utume kwa ujumla uliofanywa na Mapadri hao katika Parokia pamoja na Taasisi mbalimbali jimboni humo, hasa katika malezi yao ya kuwapeleka watu kwa Mungu.
Naye Askofu Msaidizi wa Jimbo hilo, Mhashamu Henry Mchamungu, akiwasilisha salamu za Askofu Mkuu, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, aliwapongeza Mapadri hao kwa Jubilei yao ya Miaka 25 na 50, huku akiwapongeza kwa kazi kubwa wanazozifanya katika utume wao.
Askofu Mchamungu alibainisha kwamba hakuna mtu yeyote duniani mwenye mamlaka au uwezo wa kumwondolea mtu Daraja Takatifu la Upadri, bali binadamu anao uwezo wa kumwondolea mtu hadhi ya Uklero.
“Nadhani itabidi siku moja tuboreshe lugha. Kusema miaka 25 au 50 ya Upadri kwa tukio kama hili, je utawezaje kutofautisha na tukio ambalo ni Padri ambaye hayupo katika utumishi, lakini na yeye anakumbuka kwamba ametimiza miaka 25 au miaka 50 ya Upadri?
‘Kama mnavyojua, kuna Sakrementi tatu ambazo zinaweka alama isiyofutika, ambazo ni Ubatizo, Kipaimara, na Daraja Takatifu la Upadri. Tunapoongelea kuhusu Daraja Takatifu la Upadri, ni kwamba hakuna binadamu yeyote duniani ambaye anao uwezo wa kumwondolea mtu Daraja Takatifu la Upadri, ila binadamu anao uwezo wa kukuondolea ile hadhi ya Uklero. Lakini anayekuwa Padri, anakuwa Padri milele.
Askofu huyo alibainisha kwamba neno Utumishi ni muhimu sana, na ndilo neno linalofaa kutumika kwa Mapadri, kwani linaonyesha kwamba wanapongezwa kwa miaka hiyo wakiwa katika utumishi wao, na si nje ya utumishi kama ilivyo kwa wengine.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.