Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

‘Unavyoishi ni msingi wa maisha ya mtoto wako’

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba akitoa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kwa mmoja wa vijana wa Parokia ya Mtakatifu Monika, Matosa, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kipaimara. (Na Mpigapicha wetu) Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba akitoa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kwa mmoja wa vijana wa Parokia ya Mtakatifu Monika, Matosa, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kipaimara. (Na Mpigapicha wetu)

Dar es Salaam

Na Mathayo Kijazi

Wazazi nchini wametakiwa kutambua kwamba namna wanavyoishi, na watoto wao pia wataishi kama wao.
Ili waweze kufuata maisha mema, wazazi hao wametakiwa kuishi maisha ya unyenyekevu na yenye kumpendeza Mungu, kwani watoto huiga mambo wanayofanya wazazi wao.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya kutoa Sakramenti ya Kipaimara kwa vijana 158, wa Parokia ya Mtakatifu Monica, Matosa, jijini Dar es Salaam.
“Kwa hiyo, jinsi mnavyoishi ninyi wazazi, ndivyo watoto wenu watakavyoishi, kwa sababu hatua ya kwanza ya watoto, ni kuiga yale yanayofanywa na wazazi wao,” alisema Askofu Musomba.
Katika homilia yake Askofu huyo, aliwataka wazazi kuwaonyesha njia watoto wao, ili wafahamu namna ya kuwasiliana na Mungu katika maisha yao.
Aidha, Askofu Musomba aliwasisitiza wazazi hao kuwategemeza na kuwalinda watoto wao dhidi ya mashambulizi mbalimbali yaliyopo, ili wasiharibike katika ulimwengu huu.
Aliwasihi Waimarishwa wa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kutokuwa na hofu wala woga, kwani Roho Mtakatifu waliyempokea kupitia Sakramenti hiyo, atawapa nguvu ya kuyashinda majaribu wanayokutana nayo kila wakati.
Askofu Musomba aliwataka vijana hao kutosikiliza kelele zilizopo katikati yao, bali waisikilize sauti ya Kristo pekee.
Wakati huo huo, Askofu Musomba aliwaasa vijana hao kuwa wanyenyekevu katika maisha yao, kwani ndio utakaowasaidia kuisikia sauti ya Kristo katika maisha yao.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.