Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Kardinali awatia nguvu Waamini waoga

Vijana wa Parokia ya Mtakatifu Andrea Mtume, Bahari Beach Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, waliopata Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya kupokea Sakramenti hiyo. (Picha na Yohana Kasosi) Vijana wa Parokia ya Mtakatifu Andrea Mtume, Bahari Beach Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, waliopata Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya kupokea Sakramenti hiyo. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, amawasihi Wakatoliki kuacha woga kumtangaza Yesu Kristo, kwa sababu imani ndiyo inayowasaidia maishani.
Kardinali Pengo alitoa wito huo wakati akihubiri katika Adhimisho la Misa Takatifu ya kutoa Sakrameti ya Kipaimara kwa vijana 25, wa Parokia ya Mtakatifu Andrea Mtume, Bahari Beach.
“Ndugu zangu Waamini nawaomba sana, huyu Kristo tuko naye, kwa hiyo kama yupo anayejifichaficha, aache tabia hiyo, tumtangaze Kristo, ili na yeye atusaidie katika maisha yetu:
“Utakuta watu wengine ni Wakristo wazuri sana, lakini wanapenda kuwa na tabia ya kujificha,” alisema Kardinali Pengo.
Alisema kuwa hata wakati wa kula chakula, hawapigi ishara ya msalaba, hawasali kabisa kwa sababu ya woga.
Kardinali Pengo alibainisha kuwa tabia ya Mkristo kuwaogopa watu wakati wa kuombea chakula, haifai, kwani Mkristo kamili hatakiwi kumwogopa mtu, bali anatakiwa kumtangaza Bwana Yesu Kristo mahali popote pale.
Aidha, Kardinali Pengo aliwataka vijana waliompokea Roho Mtakatifu kupitia Sakramenti hiyo kutokuwa na woga, wakamtangaze Yesu katika maisha yao.
Aliwakumbusha vijana hao kufahamu kwamba kupitia Sakramenti hiyo, wamekuwa Askari imara wa Kristo, hivyo wanatumwa kwenda kumtangaza yeye.
Kardinali Pengo alisema kuwa imani ndiyo msingi wa maisha ya kila mmoja, akiwasihi Waimarishwa hao kusali kila wakati, kwani kwa kufanya hivyo, Ufalme wa Mungu utakuwa wokovu kwao.
Kardinali aliwashukuru Waamini wa Parokia ya Bahari Beach kwa zawadi walizompatia, huku akiwapongeza kwa hatua kubwa waliyopiga parokiani hapo, ikiwemo ujenzi wa kanisa, akisema kuwa anatamani kuona ujenzi huo ukimalizika mapema, ili na yeye afike tena kwa ajili ya kusali pamoja na Waamini hao parokiani hapo.
Kwa upande wake Paroko wa Parokia hiyo, Padri Marko Loth alimshukuru Kardinali Pengo kwa kuwapatia Sakramenti vijana hao.
Naye Mwenyekiti wa Parokia hiyo, Balozi Dk. James Msekela alisema kuwa hiyo ni siku kubwa kwao kwa kutembelewa na Kardinali Pengo, akiwaomba
Waamini wa Parokia hiyo kuongeza ushirikiano ili wamalize ujenzi wa kanisa lao kwa wakati uliokusudiwa.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.