Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Askofu awatumia salamu Mapadri

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Padri Emmanuel Mushi -P.O.C.R, (kulia kwa Askofu) baada ya kupewa Sakramenti ya Upadrisho iliyofanyika Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu – Buza, jimboni humo. Kushoto ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Rainery Wolfram Mgani. (Picha na Jackson Njau) Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Padri Emmanuel Mushi -P.O.C.R, (kulia kwa Askofu) baada ya kupewa Sakramenti ya Upadrisho iliyofanyika Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu – Buza, jimboni humo. Kushoto ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Rainery Wolfram Mgani. (Picha na Jackson Njau)

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi amesema kuwa Kanisa halihitaji Mapadri wanaolaza damu katika utume wao, hivyo Padri anapopokea Daraja hilo Takatifu, anapaswa kuwa mchakarikaji katika Kanisa la Mungu.
Askofu Mkuu Ruwa’ichi alisema hayo hivi karibuni wakati akihubiri katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Daraja Takatifu la Upadri kwa Shemasi Emmanuel Mushi -P.O.C.R, iliyofanyika Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu – Buza, jimboni humo.
“Tunamwomba Mungu aliyekujalia wito wa kuwa Mtawa na kuwa Padri, akujaze Roho wake Mtakatifu, akujaze nguvu na neema, akupe mvuto na ari ya kuwa Padri mwema, Padri mwadilifu, Padri Mtakatifu, Padri mchakarikaji katika Kanisa la Mungu,” alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi, na kuongeza,
“Hatuhitaji Mapadri wanaolaza damu, na wewe ujitahidi usiwe kuwa Padri wa kulaza damu…, uwe Padri wa kujitosa, kwa sababu anayekuita anataka uwe Padri unayefurahi kuwa Padri, uliye tayari kuuishi Upadri wako kiadilifu, kuuishi Upadri wako kiheshima, kuuishi Upadri wako ukichuchumilia utakatifu.”
Aidha, Askofu Mkuu Ruwa’ichi, aliwataka waamini kumwombea Padri Emmanuel ili akue na kuimarika katika utakatifu kama Kuhani na Kasisi wa Bwana.
Wakati huo huo, Askofu Ruwa’ichi aliwasihi Wakristo kumwomba Mungu ili aendelee kuwaita vijana wengi wenye afya, akili timamu, walio watakatifu na waadilifu, ili wapokee wito wa kumtumikia Kristo ndani ya Kanisa lake kwa kuwa Mapadri.
Aliwakumbusha pia kumshukuru Mungu kwa zawadi ya Padri Emmanuel, kwani amepata wito huo si kwa mastahili yake, bali kwa mastahili ya Mungu Mwenyezi.
Padri Emmanuel ametakiwa kujibidiisha kuwakusanya waamini kuwa familia moja, ili waweze kusimama katika misingi ya kumpendeza Mungu.
Aidha, Askofu Mkuu Ruwa’ichi alilipongeza Shirika la Mapadri la Aldorin, kwa kupata Padri mpya.
Aliwashukuru wazazi wa Padri huyo kwa kumzaa, kumlea na kumtoa kwa Mungu kwa ukarimu, kwani wapo baadhi ya wazazi wasio na mtazamo sahihi, mathalani huwakataza watoto wao kutumikia miito yao.
“Kila mtoto ni mali ya Mungu… kwa hiyo kazi ya wazazi ni kuwalea watoto wao kama atakavyo Mungu, siyo kama watakavyo wao. Jifunzeni kuwalea watoto wenu ili watimize yale ambayo ni mpango wa Mungu kwa maisha yao, siyo mpango wenu kwa maisha yao,” alisema Askofu Ruwa’ichi.
Askofu Ruwa’ichi aliziasa familia zote ziwe ni kitalu cha kulea Miito Mitakatifu, kwani katika shamba la Bwana, mavuno ni mengi, ila watendakazi ni wachache.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.