Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Kanisa jipya Kibamba kutabarukiwa

Mwenyekiti wa Parokia ya Mtakatifu Vincenti wa Paulo, Kibamba, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Leonard Masige akiwaonyesha cheti cha Shukrani kutoka kwa Askofu Mkuu, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, kwa kuwa miongoni mwa Parokia 20 zilizoongoza kwa kuchangia tegemeza Tumaini Media (Kampeni ya Moyo Mt. wa Yesu, 2023). Wengine ni Viongozi wa Kamati Tendaji, na Jumuiya iliyohamasisha Kampeni. Mwenyekiti wa Parokia ya Mtakatifu Vincenti wa Paulo, Kibamba, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Leonard Masige akiwaonyesha cheti cha Shukrani kutoka kwa Askofu Mkuu, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, kwa kuwa miongoni mwa Parokia 20 zilizoongoza kwa kuchangia tegemeza Tumaini Media (Kampeni ya Moyo Mt. wa Yesu, 2023). Wengine ni Viongozi wa Kamati Tendaji, na Jumuiya iliyohamasisha Kampeni.

DAR ES SALAAM

Na Editha Mayemba

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, anatarajiwa kuadhimisha Misa Takatifu ya kutabaruku kanisa jipya la Parokia ya Mt. Vincent wa Paulo, Kibamba, Septemba 23 mwaka huu.
Akizungumza katika mahojiano maalum, Katibu wa Parokia hiyo, Victor Rweyongeza, amesema kuwa Misa Takatifu inatarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi, ikiwashirikisha Mapadri, Watawa, Waamini Walei na waalikwa kutoka Parokia jirani, na Jimbo kwa ujumla.
Amebainisha kuwa maandalizi kwa ujumla yamekamilika, ikiwemo kiroho na kimwili, yaani maungamo, semina na mafundisho  kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya WAWATA, UWAKA,VIWAWA na Wanandoa, kwani siku hiyo kutakuwa na ndoa nyingi zitakazofungishwa.
Amekumbusha pia kuwa mwaka uliopita waliadhimisha Sakramenti ya Ndoa Takatifu kwa Wanandoa jozi 30, ikiwa ni maandalizi ya waamini hao kuingia katika Kanisa jipya wakiwa wametakatifuzwa.
Kuhusu ujenzi wa kanisa hilo la kisasa ulioanza mwaka 2013, Rweyongeza amesema kuwa wanafanya maandalizi ya mwisho, ikiwemo kupaka rangi ndani na nje, na kumalizia maeneo madogo madogo yaliyobaki.
Amewashukuru Waamini na watu wenye mapenzi mema kwa niaba ya Kamati Tendaji na Kamati ya Ujenzi kwa majitoleo yao na michango iliyowezesha kazi hiyo kukamilika kwa mafanikio makubwa na kwa wakati.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.