Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Kanisa Parokia Kibamba latabarukiwa

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, akiweka ubani kwenye chungu cha moto kufukiza kwenye Altare wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kutabaruku Kanisa na Altare katika Parokia ya Mtakatifu Vincent wa Paulo – Kibamba, jimboni humo. (Picha na Yohana Kasosi) Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, akiweka ubani kwenye chungu cha moto kufukiza kwenye Altare wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kutabaruku Kanisa na Altare katika Parokia ya Mtakatifu Vincent wa Paulo – Kibamba, jimboni humo. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Kanisa la Parokia ya Kibamba, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, limetabarukiwa, huku Waamini wakionywa kutotumia vibaya kanisa hilo, kwani linapotabarukiwa, linawekwa maalumu kwa ajili ya Mungu na mambo Matakatifu.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, alisema hayo wakati akihubiri katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Kutabaruku Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Vincent wa Paulo – Kibamba, jimboni humo.
“Kanisa linatabarukiwa ili liwe tu kwa ajili ya Mungu na watu wake, pamoja na mambo yote matakatifu. Hapa si mahali pa disko, disko pelekeni ukumbini. Msipafanye hapa kuwa jalala,” alisema Askofu Ruwa’ichi.
Askofu Ruwa’ichi alisisitiza kuwa kanisani si mahali pa kupumzishia mifugo, ikiwemo mbuzi wala kondoo, kwani likifanywa hivyo, hilo litakuwa jalala, badala ya kanisa.
Aliwapongeza waamini wa Parokia ya Mtakatifu Vincent wa Paulo – Kibamba, kwa moyo wa majitoleo waliouonyesha, hadi kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo.
“Wapendwa familia ya Mungu katika Parokia ya Kibamba, nianze kwa kuwapongeza kwa kazi nzuri na nzito mliyoifanya kwa kipindi cha miaika kumi. Kwa mshikamano wenu, imani yenu, mmemjengea Mungu kanisa zuri,” alisema Askofu Mkuu.
Aidha, Askofu Mkuu aliwakumbusha Wakristo kufahamu kwamba yeyote aliyebatizwa anatakiwa kutojiruhusu kuwa jalala, bali afahamu kwamba yeye ni ndugu yake Kristo.
Askofu Mkuu Ruwa’ichi aliwaasa waamini kutambua kwamba biashara yoyote yenye sura ya dhambi, Yesu Kristo haitaki, wala haiungi mkono biashara hiyo.
Katika hatua nyingine, Askofu Mkuu Ruwa’ichi aliwataka Waamini wa Parokia hiyo kutobadilisha mwonekano wa kanisa hilo, kwani tayari limeshatabarukiwa.
“Kwa hiyo, ninyi sitegemei kwamba mwakani mtapenda kuja kurefusha upande huu na upande ule, au mtakuja kulibadilisha liwe tena la shughuli tofauti. Hili litakuwa ni mahali pa sala, mahali pa ibada, mahali penu pa kumtukuza Mungu kwa miaka yote. Hivyo, tunalipa hati ya kutabarukiwa,” alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.
Kwa upande wake Paroko wa Parokia hiyo, Padri Prijo Joseph alimshukuru Mungu kwa kuwawezesha na kuwapa nguvu katika kipindi chote, hadi kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo.
Aidha, Padri Prijo alimshukuru Askofu Mkuu Ruwa’ichi kwa mawazo na ushauri aliowapatia hadi kuweza kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo lililotabarukiwa.
Vile vile, Paroko aliwapongeza Wanaparokia hiyo kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha, kwani walikuwa bega kwa bega katika kipindi chote cha ujenzi huo wa kanisa.
Naye Padri Augustine Paikkatt, Mkuu wa Shirika la MC BS (Superior General MC BS), alisema kuwa anafurahi sana kushiriki katika Adhimisho hilo la Misa Takatifu ya Kutabaruku Kanisa.
Padri Augustine aliwapongeza waamini wa Parokia ya Kibamba, kwa michango na majitoleo yao hadi kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.