Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Majaliwa azindua Hospitali ya Wilaya Unguja

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa akipata maelezo kuhusu moja ya mtambo baada ya kuzindua Hospitali ya Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini B Pangatupu, iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa akipata maelezo kuhusu moja ya mtambo baada ya kuzindua Hospitali ya Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini B Pangatupu, iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja.

ZANZIBAR

Na Mwandishi wetu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini B Pangatupu, iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja, yenye uwezo wa kuhudumia wananchi zaidi ya 100,000 kwenye Shehia 31 wilayani humo.
Akizungumza baada ya ufunguzi wa hospitali hiyo iliyogharimu Shilingi bilioni 6.7, Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa itasaidia kupunguza adha kwa wakazi wa maeneo hayo kusafiri umbali mrefu ili kupata huduma za afya.
Aliongeza pia kuwa ujenzi wa hospitali hiyo ni utekelezaji wa vitendo wa dhamira ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, ya kuhakikisha anawekeza katika sekta ya afya kwa ajili ya ustawi wa jamii.
“Ni dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na maono ya Mheshimiwa Dkt Hussein Mwinyi ya kuimarisha miundombinu ya sekta ya afya, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma katika mazingira bora na kwa viwango vinavyokubalika,”alisema Majaliwa.
Majaliwa alisema kuwa hospitali hiyo itasaidia upatikanaji wa huduma bora za matibabu, hususan huduma za kibingwa, ambazo hutolewa kuanzia ngazi ya hospitali ya Wilaya.
“Miundombinu iliyopo katika hospitali hii, itawezesha kambi za matibabu ya huduma za kibingwa na kibobezi kufanyika hapa kwa mafanikio makubwa, badala ya kufanyika katika hospitali za mjini tu.”
Aliiagiza Wizara ya Afya ifanye tathmini ya kina ya mahitaji ya hospitali hiyo pamoja na kuhakikisha inapangiwa wafanyakazi wa fani zote wanaohitajika kwa mujibu wa kada zao, wakiwemo madaktari, wauguzi pamoja na wataalamu wengine.
Aidha, aliwataka watumishi wa sekta ya afya waendelee kufanya kazi kwa uadilifu na kujitoa. “Kuwa na majengo na vifaa tiba ni sehemu moja, lakini ubinadamu, upendo na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi, ni muhimu katika kuboresha huduma bora kwa wananchi.”
Kwa upande wake Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema kuwa katika kipindi cha miaka 60 ya Mapinduzi, idadi ya vitanda vya kulaza wagonjwa vimeongezeka kutoka 1,445 hadi 2,645, idadi ya majengo ya wagonjwa mahututi zimeongezeka kutoka sadaruki (Intensive Care Unit: ICU) moja hadi 14, vyumba vya upasuaji vimeongezeka kutoka 11 hadi 35, kati yake 13 ni kwa ajili ya akinamama, pia vitengo vya huduma za dharura vimeongezeka kutoka viwili hadi 13.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.