Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Askofu ataka watu kuzaa watoto wengi

Waamini wa Parokia ya Bikira Maria wa Mlima wa Karmeli, Bunju, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara iliyoadhimishwa parokiani hapo. (Picha na Yohana Kasosi) Waamini wa Parokia ya Bikira Maria wa Mlima wa Karmeli, Bunju, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara iliyoadhimishwa parokiani hapo. (Picha na Yohana Kasosi)

Dar es Salaam

Na Mathayo Kijazi

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, amewataka wazazi nchini kuendelea kutimiza wajibu wao katika kufanikisha mpango wa Mungu wa kuzaliana na kuijaza Dunia.
Askofu Mchamungu alitoa wito huo hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Utoaji wa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Kalmeri, Bunju, jimboni humo.
“Siku hizi wapo watu wa baadhi ya Mataifa Duniani, wanaohangaika kwa nchi zao zikiwa hazina watoto…nguvu kazi imekwisha kutokana na kuzaa mtoto mmoja mmoja, ama kuzuia uzazi. Hii ni mbaya, na ni kwenda kinyume na mpango wa Mungu,” alisema Askofu Mchamungu.
Alisema kuwa Wanaparokia ya Bunju wamejitahidi kwa wazazi kutimiza wajibu wao katika kufanikisha mpango wa Mungu kwa kuzaa watoto wengi, kwani katika Misa hiyo imeshuhudiwa wazi kwamba zaidi ya watoto 200 wamepokea Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, na hiyo ni ushahidi tosha kwamba wanaijaza Dunia.
Askofu Mchamungu alisema kuwa ni jambo la kutia moyo kuona baadhi ya wazazi wamekuwa wakitimiza wajibu huo kikamilifu, kwani mpango wa Mungu wa kuwaweka wanadamu Duniani, ni kuutiisha Ulimwengu na kuijaza Dunia kwa njia ya kuzaliana.
Aidha, Askofu huyo alisisitiza kwamba mataifa mbalimbali Duniani ambayo yamepiga vita uzazi, matokeo yake kwa sasa wanahangaika kutokana na madhara makubwa ya kupungua kwa nguvu kazi ya Taifa kwa sababu ya kutowepo watoto.
Aliwasihi wazazi kuachana na mambo ya kuiga ya kuzaa mtoto mmoja kwa kuiga mataifa mengine, akionya kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mpango wa Mungu kuhusu uzazi.
Askofu Mchamungu aliwataka wazazi kujitahidi kuwalea watoto wao katika misingi ya kiimani, na kuwaimarisha kiroho ili kuandaa jamii bora na Taifa bora la baadaye.
Katika hatua nyingine, Askofu Mchamungu aliwapongeza waamini wa Parokia ya Bunju kwa hatua kubwa ya kujenga kanisa kubwa, alilosema kwamba endapo litakamilika, litakuwa kubwa kuliko lo lote katika Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, na hilo wanaweza hata kuliita Basilika.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.