Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Kard. Pengo awaombea Barabara Tagaste

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, akifurahia zawadi aliyopewa na Wanakwaya wa Shirikisho wa Parokia ya Mtakatifu Ambrose, Tagaste, baada ya kumpongeza kwa Jubilei ya Miaka 25 ya Ukardinali. Kulia alieshika picha ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Onesmo Ngonyani. (Picha na Yohana Kasosi) Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, akifurahia zawadi aliyopewa na Wanakwaya wa Shirikisho wa Parokia ya Mtakatifu Ambrose, Tagaste, baada ya kumpongeza kwa Jubilei ya Miaka 25 ya Ukardinali. Kulia alieshika picha ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Onesmo Ngonyani. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini Tanzania (Tanzania Rural and Urban Roads Agency: TARURA), Mkoa wa Dar es Salaam, umeombwa kujenga kwa kiwango cha lami, barabara yenye urefu wa kilometa tatu kutoka Barabara Kuu ya Morogoro kuelekea katika Parokia ya Mtakatifu Ambrose, Tagaste, Jijini Dar es Salaam, ili kuwaondolea kero ya usafiri wakazi wa maeneo hayo.
Rai hiyo imetolewa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo hilo, wakati akizungumza katika Adhimisho la Misa Takatifu ya kutoa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara iliyoadhimishwa hivi karibuni parokiani hapo.
“Mmejitahidi kufanya vizuri, ila barabara imekuwa ngumu kwangu na kwa wengine kufika hapa kanisani. Hivyo basi, Viongozi mngezungumza na Mbunge mmwombe walau atengeneze kwa kiwango cha lami,” alisema Kardinali.
Aidha, aliwaomba Viongozi wa Halmashauri ya Walei wa Parokia kuchukua jukumu hilo ili kufanikisha ujenzi wa barabara hiyo.
Awali akihubiri katika Adhimisho la Misa Takatifu ya kutoa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara katika Parokia hiyo, Kardinali Pengo aliwataka Wakristo kuepuka kujilinganisha na Mungu, kwani wengi wanafanya mambo yao kwa kujiamulia wenyewe bila kumshirikisha Mwenyezi katika maisha yao.
“Kujaribu kujilinganisha na Mungu wakati wewe ni kiumbe wake, ndiko kulikotuponza sisi wanadamu tangu wazazi wetu wa kwanza. Hatutaki kumwachia Mwenyezi Mungu nafasi yake kwamba yeye aliyetuumba, ndiye aamue kwamba kipi ni kizuri kwetu, na kipi hakifai kwetu kutenda,” alisema Kardinali Pengo.
Alisema kuwa wanataka kujikana na Mungu, wanataka wawe sawa na Mungu, na wajiamulie wenyewe yale wanayotaka kufanya, matokeo yake, ndiyo vurugu zinazojitokeza kwa sasa.
“Tukigundua mfano wa dhati kabisa, Mwenyezi Mungu alipomuumba mtu, alimuumba mtu mume na mtu mke, na akasema ‘nendeni mkaongezeke’, leo hii unaona watu wanasema ‘mimi mwanaume siyo lazima nikae na mwanamke, mimi nakaa na mwanaume mwenzangu,” alisema Kardinali Pengo, akionya ukengeufu wa wandamu.
Kwa mujibu wa Kardinali Pengo, kitendo cha wanadamu kutompatia Mungu nafasi yake katika maisha yao, ndiko kunakowafanya waingie kwenye dhambi.
Aidha, Kardinali Pengo aliwataka Wakristo kufahamu kwamba Mungu ndiye mwenye kauli, na si vinginevyo, kwani wao kazi yao ni kujikusanya kwa pamoja ili wamwombe awaondolee hofu, na kuwapa ujasiri wa kuitangaza Habari Njema.
Awajaza Imani Waimarishwa Kardinali Pengo alitumia nafasi hiyo kuwasihi Waimarishwa wa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, kuhakikisha wanajikita zaidi katika imani yao, kwani wao ni Askari Hodari wa Bwana Yesu Kristo.
Kwa upande wake Paroko wa Parokia hiyo, Padri Onesmo Ngonyani alimshukuru Kardinali Pengo kwa kuadhimisha Misa hiyo Takatifu, na kumpongeza kwa Jubilei yake ya Miaka 25 ya Ukardinali.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei wa Parokia hiyo, Pius Maneno, akisoma risala katika Misa hiyo alisema kuwa Parokia hiyo ilizinduliwa na Kardinali Pengo, Januari 13 mwaka 2013, ikiwa ni Parokia ya 76 ya Jimbo hilo.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.