Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Kongamano Utoto Mt. Kondoa laibua mazito

Walezi wa Utoto Mtakatifu, Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiwa na Mwenyekiti wa Shirika la Kipapa katika picha ya pamoja, mara baada ya kupokea cheti cha ushiriki wa Kongamano la Utoto Mtakatifu Kitaifa lililofanyika Jimbo Katoliki la Kondoa. (Picha na Neema Muunga) Walezi wa Utoto Mtakatifu, Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiwa na Mwenyekiti wa Shirika la Kipapa katika picha ya pamoja, mara baada ya kupokea cheti cha ushiriki wa Kongamano la Utoto Mtakatifu Kitaifa lililofanyika Jimbo Katoliki la Kondoa. (Picha na Neema Muunga)

KONDOA

Na Bruno Bomola

Kongamano la Utoto Mtakatifu mwaka huu limefanyika kwa ustadi katika utume na hatimaye kukonga Waamini wa Jimbo Katoliki la Kondoa ambalo limepokea Msalaba kutoka Jimbo  Kuu  Katokiki la Tabora.
Kongamano hilo ambalo limekutanisha Majimbo 34, na Washiriki wa Mashirika 5515 ya Kipapa limekuwa fursa katika kuwaimarisha kiroho Waamini wa Majimbo hayo kwa njia ya semina, warsha na mafundisho ya Imani Katoliki na kuhitimishwa kwa Misa Takatifu.
Hii ni kwa mara ya kwanza kuwakutanisha watoto wa Majimbo yote kwa pamoja katika Kongamano la Kitaifa la Utoto Mtakatifu kwa mwaka huu 2023, likiwa limebeba kauli mbiu, ‘Ushirika na Utunzaji wa Mazingira’, ikiwa na mwendelezo wa Waraka wa Baba Mtakatifu Fransisko, ‘Laudato Si’, juu ya utunzaji wa mazingira.
Wamisionari hawa waliweka kambi tangu Juni 22 hadi 23 mwaka huu.
Kongamano lilifunguliwa kwa Adhimisho la Misa Takatifu na Askofu mwenyeji wa Jimbo Katoliki la Kondoa, Mhashamu Bernardin Mfumbusa, akishirikiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Mhashamu Damian Dallu, na Askofu wa Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi, Mhashamu Filbert Mhasi.
Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu, Jimbo Katoliki la Kondoa limetimiza miaka 11, huku jimbo hilo likiundwa na wilaya za Chemba na Kondoa, na wakazi wake ni Warangi, Wasandawe, Waburunge, Wagogo, Wamburu, Wabarbaigi na Watanzania wengine wanaoishi Kondoa.
Wamisionari kutoka Majimbo yote wakiongozwa na kauli mbiu ya Utunzaji wa Mazingira, wamepata nafasi ya kupitishwa kwenye semina mbalimbali juu ya umuhimu wa ikolojia na utunzaji wa mazingira, ili kuutiisha ulimwengu kama ulivyo mpango wa Mungu.
Aidha, katika kuhakikisha Watoto wanakuwa na ustawi bora wa malezi, walipata nafasi ya kupewa mafunzo ya malezi kutoka kwa Paschal Maziku na Melania Maziku juu ya haki na wajibu wa mtoto, na kukemea matumizi ya vidhibiti mimba na unyanyasaji wa kijinsia.
Katika kuhakikisha Watoto wanaendelea kupata mafunzo endelevu, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Mhashamu Gervas Nyaisonga alizindua kitabu cha Malezi ya Mtoto, kilichoandaliwa na Sista Annagladnes Mruma.
Akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu siku ya pili ya Kongamano hilo, Askofu wa Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi, Mhashamu Filbert Mhasi aliwataka Wamisionari hao kufikiri na kuwa na hekima ya kuhubiri katika utunzaji wa mazingira.
“Tunapowaona Watoto, tunakuwa na matumaini makubwa sana na ninyi mtaenda kuinjilisha, na tena mtakuwa wainjilishaji wazuri juu ya utunzaji wa mazingira ambayo ni nyumba yetu nzuri sana, na nyumba yetu pendwa sana,” alisema Askofu Mhasi.
Juni 25 mwaka huu, Kongamano la Utoto Mtakatifu Kitaifa lilihitimishwa kwa Adhimisho la Misa Takatifu iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Mhashamu Damian Dallu, na Homilia ilitolewa na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Mhashamu Garvas Nyaisonga.
Katika homilia yake, Askofu Nyaisonga aliwataka Wamisionari hao kutokuwa na hofu wala ubinafsi, badala yake wawe na fadhila ya ushirika kwa kuwatendea wengine matendo mema, bila kujali hali zao.
Aidha, Nyaisonga alisema kuwa Dunia kuna wakati inakosa usikivu kwa sababu ya kuambiwa mengi na kushindwa kuyapokea kwa usikivu, na akawataka Watoto wamisionari kuwa wasikivu kwa wazazi, walezi, waalimu na Viongozi wa Dini.
Ni kama Yesu alivyopokelewa Yerusalemu, ndivyo ambavyo maandamano yalivyopokelewa na wenyeji wa Kondoa. Waamini Wakristu na wasio Wakristu waliungana katika maandamano wakizunguka Mji wa Kondoa kumtangaza Kristu, na huu ndio Umisionari.
Hivyo ndivyo watoto 5515 wa Shirika la Kipapa wakisindikizwa na walezi wao kutoka Majimbo 34 ya Kanisa Katoliki Tanzania, walivyofanya uinjilishaji katika Jimbo Katoliki la Kondoa, huku tukisubiri tena kutangaziwa Jimbo litakaloandaa Kongamano lijalo la Kitaifa.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.