Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Mjadala wa Bandari na hadithi ya Punda wa familia

MWANZA

Na Paul Mabuga

Katika kupatana biashara baadhi ya Waswahili, kwa maana halisi ya kiarabu, watu kutoka Pwani, hasa wazaramo, wanaongozwa na dhana kuwa, kwa mwali kuliwe na kwa kungwi kuliwe.

Dhana hii huwaongoza katika mwelekeo wa kamba  ili  kufanikisha  mapatano ya biashara  ni lazima kukubali kupoteza kidogo kwa mdaawa [the party] ili upate zaidi.

Ukifika hapa unafikiria, ingekuwa Wazaramo kama wataongozwa dhana hii wangesema nini kuhusu mtazamo wao katika mjadala kuhusu kile kinachoendelea katika makubaliano ambayo yana lengo la kupata mwekezaji wa kuiendeleza Bandari ya Dar es Salaam.

Hasa kwa sababu kuna pande nyingi zinavutana huku kila mmoja ukijinasibu kuwa sahihi, lakini mwisho hatimaye wana mzizima katika utajiri wao wa lugha wanatuambia kama tunataka kufaidika katika hatua ya kuelekea uendelezwaji wa Bandari ya Dar es Salaam  ni lazima kwa mwali kuliwe na hali kadhalika kwa kungwi!

Tunahitaji kuivuna vya kutosha bandari yetu ili kupata rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Kama ilivyo kawaida, tuna watu, ardhi na rasilimali za asili lakini hatuna mtaji, teknolojia  na utaalam ambao kwa changamoto inayotukabili ni  lazima utoke kwa kungwi!

Wazaramo wanatuambia kwamba lazima tukubali kupoteza sehemu ikiwa tunataka kufanikiwa zaidi. Anayekuja kuwekeza anashida zake na sisi mwali wetu naye ana shida zake.

Ila kwa mijadala, misimamo na ushauri unaotolewa na makundi mbali mbali kwa watoa maamuzi, unatupa hadithi nyingine.

Hii ni hadithi ya familia iliyokuwa inataka kwenda kumuuza punda wa familia kwa ajili ya kupata fedha, kama rasilimali kwa ajili ya kutatua changamoto waliyokuwa nayo, pengine kama sisi ilivyo na bandari yetu.

Katika kufanikisha hilo familia ikamchagua Baba na Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 15 kweda kumuuza punda huyo mnadani.

Kwa kuwa mnada ulikuwa mbali iliwabidi kusafiri kwa kutembea na punda wao huku njiani wakikutana na watu wa aina mbali mbali. Wao wakitembea na Punda pembeni yao.

Walipofika mahali fulani, mmoja wa watu aliokutana nao, akawaambia baba, mbona unamtembeza huyu mtoto, atachoka, maane yeye siyo mtu mzima na hawezi kuhimili mwendo mrefu.

Kwamba mwendo mrefu utamuathiri afya yake na hivyo ni   akheri mtoto apande juu ya punda na safari iendelee ili kumuokoa na madhila yanayoweza kumpata.

Baba akachukua ushauri ule na mtoto akapanda juu ya punda huku yeye akitembea kwa miguu na wakaendelea na safari kuelekea mnadani.

Kama ilivuo katika siku za mnada watu huwa wengi na mifugo yao kuelekea katika mahali ambako kuna siku ya soko.

Wakiwa safarini, wakakutana na jamaa mwingine tena ambaye yeye aliwasimamisha na kuwaambia, kulikoni, kijana ambaye  anatakiwa kujengwa kwa utu wema na nguvu ndiyo apande punda ilihali baba yake  anatembea. Yule jamaa akasema huko siko kumfunza vema mtoto na ni kumkosesha adabu.

Wakausikia ushauri na mtoto akateremka na Baba akapanda punda na safari inakendelea. Wakiwa njiani wakakutana na mtu mwingine  ambaye yeye aliwauliza kwamba, huyo punda wanakwenda kumuuza au wanamtumia kwa usafiri? Baba akajibu, Naam, tunakwenda kumuuza.

Ndipo mtu yule akawaambia, kama ni wa kuuza, inabidi wasimpande ili afike akiwa na afya na kupata bei nzuri! Na kwamba  ingekuwa bora zaidi wangembeba punda wao hadi mnadani.

Baba na mtoto wakauchukua huo ushauri na kuendelea na safari huku wakiwa wamembeba mabegani punda yule na kuendelea na safari.Wakaendelea na safari  huku punda akiwa mabegani.

Katika njia hiyo kulikuwa na changamoto ya mto na hivyo iliwalazima kuuvuka  mto huo na punda wao mabegani ili kuendelea na safari kwenda  mnadani.

Kwa bahati  mbaya, kutokana na mto kuwa na maji yenye mwendo kasi, baba aliteleza na punda yule akaanguka  na kusombwa na maji na wasiweze kumuokoa.

Na matokeo yake familia ile ikawa imemkosa punda wa kuuza na fedha walizotegemea kupata ili kutatua shida zao zikakosekana.

Familia ikaanza kulaumiania kutokana na kufuata ushauri ambao ni kama vile uliwapoteza njia. Walifikia hatua ya kuchunguza kila aliyekuwa akiwashauri alikuwa na wasifu gani, lakini haikusaidia, ikawa imeisha hiyo.

Katika jambo letu la Bandari kuna kila aina ya ushauri, kuna idadi ya makundi kadhaa yanayohusika na pia ni wazi kuwa karibu kila moja linaonekana likiwa na chanzo chake cha hamasa kufanya hivyo.

Bahati nzuri karibu moja kati ya makundi hayo na ushauri unaotolewa unalenga kumfikisha punda mnadani.

Pengine cha kujiuliza ni kuwa je, msimamo uliopo na ushauri unaotolewa utatusha mtoni na tukafika mnadani na kupata kile ambacho tumedhamiria kukipata na kunufaika kama taifa na wananchi.

Lakini pia ifahamike kuwa kwa eneo la kimkakati ambalo Bandari ya Dar es Salaam ipo, na kama ilivyo katika maeneo megine, kama reli ya kati, Bwawa la Mwalimu Nyerere  na hata bomba la Mafuta ghafi kati ya Uganda na Tanzania, limekuwa na  changamoto ya kushambuliwa kiushindani na hata watu wa nje  na watanzania wanapaswa kujitambua katika hili.

Tunahitaji kuwa makini ili Bandari hii iwe aina ya rasilimali bora itakayotupatia manufaa watanzania kwa ujumla.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.