Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA), Parokia ya Kristo Mfalme – Tabata, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakishangilia moja ya matukio wakati ya Sherehe yao WAWATA Day Kiparokia, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu. (Picha na Yohana Kasosi)

Waandishi wa Habari wakiwa kanisani wakifuatilia Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Wanamawasiliano, iliyoadhimishwa katika Parokia ya Bikira Maria Mama wa Fatima – Msimbazi, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. (Picha na Mathayo Kijazi)

Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kristo Mfalme – Tabata, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Bonaventure Kisoka akizindua mashine ya mazoezi iliyonunuliwa na Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) wa Parokia hiyo wakati ya Sherehe ya WAWATA Day kiparokia. (Picha na Yohana Kasosi)

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba (aliyeshika fimbo ya Kichungaji), akiwa katika picha ya pamoja na Wanandoa wa Parokia ya Mtakatifu Paulo Mtume - Kisegese, Rufiji mkoani Pwani, jimboni humo, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Sikukuu ya Somo wa Parokia hiyo, iliyoadhimishwa parokiani hapo. Kulia kwa Askofu ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Gaspar Bolongola. (Picha na Yohana Kasosi)

Wanamoyo Mtakatifu wa Yesu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam na Jimbo Katoliki la Moshi, wakisali mbele ya sanduku lililobeba mwili wa Mwanashirika mwenzao, marehemu Theresia Nicholaus Massawe wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kumwombea, iliyoadhimishwa kijiji cha Maua Kati wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro. (Picha na Yohana Kasosi)

Dar es Salaam

Na Mwandishi wetu

Wanajumuiya wametakiwa kulishika na kuliishi Neno la Mungu kwa ukamilifu bila kuwa na hofu yoyote katika maisha yao ya kila siku.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Padri Bonaventure Kisoka, Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kristo Mfalme – Tabata, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Mtakatifu Fabiano, parokiani hapo.
“Waamini muwe watu wa kusali kila mnapokutana, kwa sababu ninyi ni Wakrito, mnapoishi kwa umoja msije mkatengana, endeleeni kusali pamoja kama hivi leo mnaposherehekea Sikukuu yenu mmeungana kitu kimoja, hivi ndivyo inavyotakiwa Wakristo,”alisema Padri Kisoka na kuongeza,
“Tambueni kwamba Jumuiya ni kanisa ndogo la nyumbani, mnakuwa Wakrito wenye umoja. Endeleeni kusali pamoja kama hivi kila wakati, mfuateni Mtakatifu wenu wajumuiya, Mtakatifu wenu alikuwa mtu mwema ambaye alimsikiliza sana Mungu, na ninyi muwe watu wema.”
Aidha, aliwasihi kuungana kwa pamoja ili waweze kuwa na furaha katika Jumuiya yao, Kanda, pamoja na Parokia yao ya Kristo Mfalme, kwa ujumla.
Padri huyo aliwasihi Waamini wenye tabia za kujilimbikizia uongozi, waache kufanya hivyo, akisema kwamba baadhi yao wakipata uongozi, wanajiona ndiyo wameshafanikiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya Mtakatifu Fabiano, Alfred Kunambi alisema kuwa kwa sasa Jumuiya yao ni changa ina miezi michache tangu Paroko wa Parokia hiyo awatangaze, bali wanaishi Ukristo wao kwa furaha.
Kunambi aliongeza kuwa mwaka huu mpya, Jumuiya yao imejipanga vyema, hasa katika mavuno ya Parokia na Jimbo, pamoja na kushiriki katika michango mbalimbali wanayoambiwa na Parokia yao.
Hata hivyo, aliwaomba Viongozi wa Vyama vya Kitume kila Parokia na Parokia Teule, kumuunga mkono Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi kwa kutoa michango yao ili kukamilisha ujenzi wa Kanisa Kuu Mbadala la Gezaulole.

MOSHI

Na Mwandishi wetu

Watanzania wametakiwa kutoruhusu Vyama vya Siasa viwagawe na kuwafanya watengane kwa itikadi hizo, kwani sifa kubwa ya Taifa hilo, ni kuwa na amani.
Hayo yalisemwa na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bikira Maria Mshindaji, Jimbo Katoliki la Kigoma, Padri George Muhanuka wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kumuombea marehemu Theresia Nicholaus Massawe, iliyofanyika Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni – Kibosho- Singa, Jimbo Katoliki la Moshi.
Aidha, Padri huyo aliwasihi Waamini kuwa wamoja, huku wakiachana na tabia ya ubinafsi katika imani yao.
“Waamini, tujitahidi kuwa wamoja, tuachane na tabia ya ubinafsi katika imani. Lakini pia Vyama vya Siasa CCM, CHADEMA, au chama chochote kile, visitugawe katika umoja wetu tukiwa Watazania wenye amani,” alisema Padri Muhanuka.
Padri Muhanuka aliongeza kwa kusema, “Ndugu zangu Waamini tujiandae, hatujui muda wala saa tutakapoitwa na Mungu, maana tunakuwa Waamini wa Jumapili tu, wala hatupo kama Waamini wa kuwa na Mungu karibu.”
Padri huyo alisema pia kuwa Theresia Massawe enzi ya uhai wake, aliuishi Ukristo wake kwa imani moja ya Kanisa Katoliki, ambaye pia alikuwa mwanashirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu, na alijiunga pia na Shirika la Mtakatifu Anna.
“Je, wewe Mwamini umejiunga na chama gani cha Shirika la Kanisa? Jitathmini Ukristo wako unaoishi kwa sasa, Mungu ametuleta hapa duniani ili tumtambue na tumtumikie, ili siku ikifika, tuwe mahali pa wokovu. Huyu mama aliishi kiukamilifu bila shaka lolote,” alisema Padri huyo.
Alibainisha pia kuwa Waamini wengi hawauishi Ukristo wao kikamilifu, kwa sababu ya kutangatanga katika Makanisa mbalimbali kutafuta miujiza.

DAR ES SALAAM

Na Jonas Abel

Mamlaka ya Mapato Tanzania (Tanzania Revenue Authority: TRA), imesema kuwa mfumo mpya wa Tanzania Customs Integrated System (TANCIS), utarahisisha uingizwaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi na kuingia ndani kwa haraka, jambo litakalosaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na watafanyakazi mchana na usiku.
Mfumo huo uliozinduliwa hivi karibuni, umebuniwa ili kuboresha ufanisi, kuhakikisha usahihi, na kupunguza ucheleweshaji katika shughuli za forodha.
Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Forodha, Januari 26 mwaka huu, yenye kaulimbiu “Forodha itatimiza ahadi yake ya usalama na ustawi”.
Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda alieleza maboresho makubwa yaliyofanywa kwenye mfumo huo alisema,
“Mfumo mpya wa TANCIS unatumia teknolojia ya akili bandia kwa ajili ya uchakataji wa data kwa usahihi, uwazi zaidi, na urahisi wa operesheni…TRA tumejipanga kuboresha mifumo yetu na taratibu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuboresha shughuli za forodha.”
Alisema kwamba mfumo ulioboreshwa, ambao ulianza kufanya kazi rasmi Januari 20, 2025, umekumbana na changamoto ndogo wakati wa uzinduzi wake wa awali. Hata hivyo, Kamishna Mkuu (Commissioner General) aliwahakikishia wadau kuwa mafundi wanashughulikia changamoto hizo kwa bidii.
Alisisitiza pia kuwa mfumo mpya utapunguza kwa kiasi kikubwa ucheleweshaji wa ukaguzi wa mizigo na gharama zisizo za lazima, hivyo kuboresha ufanisi kwa ujumla.
“Ahadi yangu, pamoja na timu yangu, ni kuwa kuanzia Februari, mfumo huu ulioboreshwa utaanza kufanya kazi kikamilifu na kuwafaidisha watumiaji wote,” alisema, akibainisha kuwa maboresho hayo pia yatahakikisha thamani ya bidhaa inakokotolewa kwa haki na usahihi zaidi.
Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Edward Urio, alionyesha matumaini kuhusu mfumo mpya wa TANCIS, akipongeza uwezo wake wa kuboresha ufanisi na uwazi katika ukusanyaji wa mapato.
“Tunaamini mfumo huu utaongeza uwazi na ufanisi,” amesema Urio. Hata hivyo, amekiri kuwa baadhi ya wanachama wamekumbana na changamoto, kama vile gharama za ziada kutokana na ucheleweshaji wa kuhifadhi na kusafirisha mizigo wakati wa awamu ya awali ya utekelezaji wa mfumo huo.
Kwa upande mwingine, Kamishna wa Forodha, Juma Bakari alisema kuwa mfumo mpya wa ukaguzi wa bidhaa umeboreshwa zaidi ukilinganisha na ule wa awali uliotumika tangu mwaka 2014.
“Unarahisisha shughuli za kibiashara, hasa katika uagizaji na usafirishaji wa bidhaa,” alisema Bakari.
Alibainisha pia kuwa mfumo huo unaziunganisha taasisi 36 zinazoweza kuutumia, hivyo kuboresha mawasiliano kati yao.
Aidha, alisema kwamba kutakuwa na matumizi bora ya taarifa, kwani data zitasimamiwa vizuri, hivyo kusaidia maafisa wa forodha na taasisi nyingine kufanya maamuzi sahihi.
Mfumo mpya wa TANCIS ni hatua muhimu katika kuboresha taratibu za forodha nchini Tanzania, kuhakikisha taifa linaendelea kufanikisha malengo yake ya usalama na ustawi.

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Wakili wa Kujitegemea Dk. Aloys Rugazia amesema eneo la jinai la kubambikiwa kesi ni eneo linalosumbua watu wengi katika jamii.
Amesema kuwa Wananchi wamekuwa wakilalamika kwamba hiyo ni changamoto wanayokutana nayo katika maisha yao.
Dk Rugazia (pichani) alisema hayo katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar es Salaam wakati wa maandalizi ya kutoa elimu ya sheria bure na kuandaa nyaraka katika kuadhimisha wiki ya sheria kwa lengo la kuwafikia wananchi ambao hawana fedha za kupata huduma za sheria.
“Tunapokutana na wananchi wanatueleza changamoto nyingi katika eneo la jinai kwamba kuna kubambikiwa kesi kuna kuonewa ndiyo maana tunawataka waje hapa tuwape elimu ya kutosha wajue haki zao ni zipi na watakiwa kufanya nini,” alisema Dk. Rugazia
Aidha, alisema changamoto nyingine ambayo wananchi wanapata ni eneo la ardhi na mirathi wajane, wazee na watoto yatima wanapata shida kupata haki zao za msingi kwa wakati.
“Ardhi ni maisha ni moja kati ya mali muhimu katika mustakabali wa watu mara nyingi ardhi imekuwa ikileta msuguano waliyonacho na wasio nacho, mara nyingi wanajikuta katika hali ngumu ndiyo maana kwa wiki hii tunatoa msaada bure watu waje,” alisema Dk. Rugazia.
Aliongeza kwamba wapo kwenye wiki ya sheria ambayo ilizinduliwa Januari 25, 2025 kwa kawaida wanaadhimisha kwa kujaribu kuifikia jamii kuhakikisha inapata haki kwa sababu sio kila mtu anauwezo wa kulipia gharama za kupata huduma za kisheria.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni alianzisha mpango maalumu wa kusaidia wananchi wa Mama Samia Legal Aid, mkakati wa kutoa msaada wa kisheria kwa watu wanaishi kwenye jamii wenye kiu ya kudai haki ambao hawawezi kuipata.

Kisarawe

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Viwanda Dk. Selemani Jaffo ameiagiza Mamlaka ya Maji Vijijini (Ruwasa) kuchimba Kisima kirefu Kata ya Bwama iliyopo Wilayani Kisarawe, Mkoani Pwani.
Dk. Jaffo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe alitoa agizo hilo alipofika Bwama kwenye kuzindua Zahanati ya Bwama iliyogharimu Shilingi milioni 77/- hadi kukamilika kwake tangu ujenzi ulipoanza mwaka 2010.