Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba- OSA, amewataka Waamini kuachana na tabia na mazoea ya kushiriki na kupokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu bila kujiandaa.
Wito huo aliutoa hivi karibuni wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Uzinduzi wa Kigango kipya cha Kuzaliwa Bikira Maria – Kisukuru, Parokia ya Roho Mtakatifu - Segerea, jimboni humo.
“Mkristo lazima ujitakase ukiwa msafi wa roho ili ushiriki chakula cha Bwana. Huyu ni Mungu, lazima ujinyenyekeze kwake ukiwa mkamilifu. Wakristo muwe watu wa kujitakasa muda wote kwa sababu, isipojiandaa mkiwa wenye usafi wa Roho na wenye Imani Moja Takatifu ya Kristo, lazima mjichunguze kwanza mnaishije hapa Duniani kwa imani hii ya Ukristo wenu. Ndugu zangu Waamini, huu Ukristo tuutumie vizuri, maana ndiyo njia yenye ukweli wa kutuongoza katika maisha yetu,” alisema Askofu Musomba.
Aidha, Askofu huyo aliwasihi Waamini wenye tabia ya kutoa mimba au kuzuia ili wasipate mimba, watambue kwamba wametenda dhambi mbele za Mungu.
“Waamini wenye kutoa mimba au kuzuia wasipate mimba wajue kwamba wametenda dhambi kubwa, wameua. Kwa hiyo msifanye hivyo. Wale wenye tabia hiyo, Mungu amewaleta ninyi hapa duniani ili mumtumikie na umtambue, kwa nini ninyi leo mnamzuia mwenzenu wasizaliwe? Acheni kabisa kufanya hivyo,” alisema Askofu Musomba.
Vile vile, aliwaasa Waamini kujiandaa vyema kwa ajili ya kumpokea Masiha, wakitambua kwamba Masiha anazaliwa kwa ajili yao, hivyo wawe tayari kwa ajili ya mapokezi yake, huku wakiwa wasafi wa mioyo, pamoja na kuachana na tabia ya kuwa watu wa chuki.
“Mama Bikira Maria alipopewa taarifa kuwa ni mjamzito, utazaa mtoto mwanaume ingawa alishangaa pia alishtuka, lakini alipokea kwa imani moja kubwa, je, wewe mama leo ungeambiwa hivi ungesema nini? Tuwe watu wa imani kupokea kitu kwa unyenyekevu na furaha, huku tukiwa watu wa imani na unyenyekevu mkubwa,” alisema Askofu huyo.
Askofu Musomba aliwaasa Wanakigango hicho kuwa watu wa kupendana na kuheshimiana, kwani wakifanya hivyo, watafika mbali kimaendeleo katika Kigango chao.
“Mkifanya hivyo, mtafika mbali katika Kigango hiki, ili mje mfikie kuwa Parokia kamili. Mtambue kwamba hakuna Kigango kinachozinduliwa na Askofu, Kigango huwa kinazinduliwa na Paroko tu, lakini ninyi leo mmepata bahati kubwa sana kuzinduliwa na mimi Askofu, msiniangushe, mjitahidi kukua haraka, mjenge kanisa kubwa pia mjenge nyumba ya Mapadri haraka sana...
“Nimefurahishwa sana na makubaliano yenu ninyi Maparoko wawili katika Parokia hizi mbili, Parokia ya Makoka na Parokia ya Segerea, mmetoa Jumuiya zenu na kuunda Kigango, mmefanya vizuri sana, huu ndio Ukristo unaotakiwa, siyo kuwa na malumbano,” alisema Askofu.
Askofu Msaidizi, Mhashamu Stephano Musomba alitangaza kuwa Kigango hicho kitahudumiwa na  Mapadri wa Parokia ya Roho Mtakatifu, Segerea.
Kwa upande wake Paroko wa Parokia hiyo ya Segerea, Padri Denis Kunambi aliwaomba Waamini wa Kigango kipya wampe ushirikiano ili waweze kufikia maendeleo zaidi katika Kigango hicho.
Padri Kunambi alisema kuwa Kigango hicho kimezaliwa kwa baraka kubwa, kwa sababu eneo hilo lilinunuliwa na Parokia ya Segerea kwa lengo la kujenga shule kama mradi wa Parokia, lakini sasa wazo hilo limegeuka kuwa Kigango.
Naye Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Gaudence – Makoka, Padri Amaladoss Chinnappan aliwaasa Waamini waliotoka katika Parokia ya Makoka na kujumuika katika Parokia ya Segerea, kupitia Kigango hicho, wasichukie wala kusikitika, bali wafurahi kwa sababu wote ni Waamini Wakatoliki.
Padri Chinnappan alimshukuru Askofu kwa kuwaweka pamoja, kuwapatanisha na kuwapatia Kigango ambacho amekizindua, akiwasihi Waamini kufahamu kwamba huo ndio Ukristo wanaotakiwa kuuishi katika maisha yao ya kila siku.

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu amewataka Waamini kutokubali kuyumbishwa kiimani.
Askofu Mchamungu alitoa wito huo hivi karibuni katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara iliyofanyika Parokia ya Mtakatifu Cesilia -Kisarawe ll, Kigamboni.
Askofu Mchamungu alisema waamini wanatakiwa kuitangaza Injili kwa watu wote ili wamjue Mungu wa kweli.
“Ndugu zangu, tushike Maandiko Matakatifu… hayo ndio yatatusaidia kuona utukufu wa Mungu,”alisema Askofu Mchamungu.
Kwa upande wa Waimarishwa wa sakramenti hiyo, aliwataka kutambua majukumu yao sis i kuwasimamia watoto hao, bali hata kuwasaidia na kuwaongoza katika misingi thabiti ya kimaadili.
Askofu Mchamungu aliwataka waamini wa parokia hiyo wajenge Kanisa kwa sababu kanisa la sasa ni dogo.
Naye Paroko wa parokia hiyo,Padri Roger Kamuzinzi, aliwaomba waamini kumpa ushirikiano ili aweze kutekeeleza vyema majukumu yake ya kitume.
Padri Kamuzinzi alimshukuru Askofu Mchamungu kwa kuwapatia vijana 31 Sakramenti ya kipaimara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Parokia hiyo, Geofrey Lyungu alisema parokia hiyo bado changa kwani ina muda wa miezi sita tu tangu ilipotangazwa na Askofu Mkuu Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, kuwa Parokia Kamili.

MOROGORO

Na Mwandishi wetu

Katibu wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Padri Boniface Mliga amewataka Watawa wa Kike wa Shirika la Maria Imakulata (SMI), walioweka Nadhiri za Daima kuona fahari kwa kutoa maisha yao kama Sadaka ili kumtumikia Mungu.
Padri Mliga alisema hayo hivi karibuni wakati wa Adhimishi la Misa Takatifu ya Nadhiri za Daima kwa Masista wa Shirika la Maria Imakulata –SMI, iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli –Kihonda, jimboni Morogoro.
“Ndugu zangu, inawapasa kutambua Agano ni makubaliano, kwani hata Wana Waisraeli waliweka Agano na Mungu, nanyi mnaweka Agano kati ya Mungu na Kanisa, la kumtumikia kama kiumbe chake mwenyewe, huku mkitoa maisha yenu kama zawadi na sadaka kwake,”alisema Padri Mliga.
Aidha, aliwataka Masista hao kutenda mema na kumtumikia Kristo siku zote za misha yao, akiwakumbusha kuwa kila mtu anayehitaji kumfuata Yesu, lazima aikane nafsi yake kwa kuachana na mambo ya kidunia, na kumfuata.
Padri Mliga aliendelea kusema, “Ukiikana nafsi yako, pia unatakiwa ubebe msalaba wako.”
Aliendelea kusema  kwamba kama mtu amechagua kumfuata Kristo na kukubali, yampasa kujiuliza, je, ana uwezo huo wa kuacha  mambo yote?
“Kwani wasije kukubali kuacha ya ulimwengu, na baadaye wakashindwa na wakakata tamaa, kwani maisha ya kumfata Kristo, si maisha ya kimasihara,”alisema Padri Mliga.
Kwa mujibu wa Padri Mliga, Kristo alichekwa na kudhihakiwa na baadhi ya watu, lakini hakukata tamaa na badala yake, aliendeleza kazi yake ya kuhubiri Injili kwa mataifa, na mwishowe aliteswa na kukubali kufa msalabani, ili atimize agano lililoandikwa hapo kale.
Alitoa wito kwa Masista wamkimbilie Mungu siku zote za maisha yao, kwa kupokea msalaba na kuubeba kwa furaha na si kwa huzuni, ili waweze kukidhi vigezo vya kuwa wafuasi wa Kristo.
Mbali na hayo, Padri Mliga aliwataka watawa hao wasitazame walipotoka wala kukata tamaa, bali watazame Msalaba wa Kristo kwa imani na matumaini makubwa, kwa kujitoa zaidi, wakiomba Mungu waendelee kuubeba Msalaba wa Kristo, kwa amani na upendo.

KARONGA, Malawi
Chama cha Wanawake Wakatoliki (Catholic Women Association: CWA) nchini Malawi, kimefanya Mkutano Mkuu wa 45 wa Mwaka kuanzia Desemba 18–22 mwaka huu.
Mkutano huo ulifanyika katika Misheni ya Chaminade, Jimbo Katoliki la Karonga chini ya kauli mbiu isemayo: “Kukuza Uzazi, Njia ya Furaha ya Furaha na Utakatifu.”
Akizungumza, Mwenyekiti wa CWA Taifa, Doreen Banda Zimba alisema kuwa maandalizi yalikuwa yakiendelea vizuri, akitolea mfano shughuli za kamati ndogo.
“Kila kamati, ikiwa ni pamoja na zile za itifaki, liturujia, malazi, afya, na usafi wa mazingira, miongoni mwa zingine, ziko chini kuhakikisha kwamba kila kitu kinawekwa kabla ya muda uliopangwa,” alisema.
Aliongeza kuwa wanawake kutoka kila Jimbo walijitolea kufanya maandalizi ya usafiri wa kuwapeleka kwenye eneo la mkutano.
Mazungumzo mengine yalihusu mada, kama vile asili na madhumuni ya ndoa na familia, Kanuni Nne za Mafundisho Jamii ya Kanisa, Kiroho cha CWA, na Uongozi Kanisani, na Maoni ya Kitamaduni na Kisheria kuhusu Utoaji Mimba na Muungano wa Jinsia Moja, miongoni mwa mambo mengine.
Mawasilisho hayo yaliwezeshwa na Maaskofu, Mapadre na Walei, ambapo Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Malawi, Mhashamu Askofu Mkuu George Desmond Tambala, aliongoza liturujia ya ufunguzi katika Mkutano huo.

KASESE, Uganda

Padri Raphael Balinandi Kambale ameadhimisha Jubilei ya Dhahabu katika Parokia ya Nsenyi, Jimbo Katoliki la Kasese nchini Uganda, akiwasihi Mapadri vijana na Wakristo kwa ujumla, kujenga upendo kwa Kanisa, na kujitolea kwa ajili ya Miito.
Padri Balinandi, ambaye kwa sasa ni Padri mzee zaidi katika Jimbo Katoliki la Kasese, alipewa Daraja Takatifu la Upadri, Desemba 14 mwaka 1974 katika Parokia ya Nsenyi na Askofu Vincent J. McCauley, mbele ya Askofu Sarapio Magambo na Askofu Kathaliko Emmanuel, kutoka Jimbo Katoliki la Butembo-Beni.
Yeye alikuwa Padri wa tatu kutoka Jimbo Katoliki la Kasese, akifuatiwa na Monsinyori Augustine Muhindo Hayati, aliyepewa Daraja la Upadri wa kwanza mwaka 1958 na Padri Louis Isingoma Byakuyamba mwaka 1972.
Katika hotuba yake muda mfupi baada ya Misa iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Kasese, Mhashamu Francis Aquirinus Kibira Kambale, Padri Balinandi alitajwa kuwa mtu wa thamani katika Jimbo na Wilaya kwa ujumla, ambaye amechangia maendeleo ya kiroho, kitamaduni na mazingira.
Askofu Francis Kibira alisema kuwa Ndoa Takatifu inachukuliwa kuwa ni Sakramenti yenye nguvu katika Kanisa Katoliki ambayo wanandoa wanapaswa kuilinda kwa wivu kwa sababu ni mfugaji wa Sakramenti nyingine.
Vile vile, Askofu Kibira ambaye alitoa wito wa mafunzo ya Katekesi miongoni mwa watoto, alisema kwamba ili Kanisa liwe na Mapadri wazuri na wanandoa miongoni mwa Miito mingine kanisani, wazazi wanatakiwa kuwa na sababu na kuweka thamani katika ndoa ili kuwalea watumishi makini wa Kanisa na Jumuiya.
Katika ujumbe wake, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Gulu, Mhashamu John Baptist Odama, mwanafunzi mwenza wa Padri Balinandi, alirejea maelezo ya watu wengine kuhusu Padri, kwamba yeye ni mtu mwenye imani kubwa kuhusu maisha kama Kasisi.
Mbali na hilo, aliendelea kwa kusema, “Nina kumbukumbu zake za kuwa na shauku kubwa ya liturujia, na kutamani sana kufuata kanuni za kiliturujia na Neno la Mungu.”
Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la Kasese, Mhashamu Egidio Nkaijanabwo alisema kuwa Padri Balinandi alikuwa mtu wa mila nzuri, na alipenda utamaduni wake.
Kupitia utamaduni wake, kujifundisha, na kupitia elimu yake zaidi, Padri Balinandi ameonekana kuwa na ujuzi katika lugha ya Lhukonzo.
Miongoni mwa umahiri mwingine, alitafsiri vitabu vingi vya kiliturujia katika lugha ya kienyeji, zaidi ya yote aliyoheshimu Ufalme wake.
Katika mahubiri yake, Padri Expedito Masereka, Msimamizi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bukangara, aliwataka Wakristo kujifunza kutoka kwa Padri Balinandi kujiendeleza kiujumla kwa kuanza na wao wenyewe.
Mratibu huyo wa zamani wa Kichungaji, alimpongeza mshereheshaji huyo kwa michango yake ya umoja, na kukuza lugha ya Lhukonzo, kazi inayowalazimu Wakristo katika Miito mingine kutimiza wajibu wao kwa umakini na matumaini, kama inavyotarajiwa hadi mwisho.
Mjubilei huyo, Padri Balinandi Kambale akiwa na furaha tele, alimpongeza Askofu Kibira kwa upendo na matunzo katika uzee wake, akisema kuwa aligubikwa na upendo, ukarimu na uangalizi alioonyeshwa na Wakristo, na watu wema.
Naye Mkuu wa Walei wa Jimbo Katoliki la Kasese, George Mayinja, aliwataka wazazi kuwalea watoto wao kulingana na huduma ya Kanisa, lakini pia kuwekeza katika Elimu yao.

LUSAKA, Zambia
Kituo cha televisheni cha Kikatoliki nchini Zambia, Lumen TV-Z kimepata msukumo mkubwa kwa kuweka mfumo wa umeme wa jua wa KVA 11 wenye thamani ya Kwacha 270,000 ambayo ni takriban dola 9,815, sawa na Shillingi 23,485,910.45/- za Kitanzania.
Mfumo wa jua uliotolewa na GEI Power Limited na kukabidhiwa rasmi hivi karibuni katika kituo hicho, unashughulikia changamoto zinazoendelea nchini za uondoaji wa shehena, na ulitolewa kama sehemu ya ahadi iliyotolewa na GEI wakati wa chakula cha mchana cha Lumen TV mnamo Septemba, ikionyesha ushirikiano unaoendelea kati ya mashirika hayo mawili.

VATICAN

Baba Mtakatifu Fransisko amewataka Waamni kusimama kidete kulinda na kutetea Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo, akiwasisitiza kupokea zawadi ya uhai kwa moyo wa upendo, shukrani na ukarimu.
Aliyasema hayo wakati wa Dominika ya Nne ya Majilio, Mwaka ‘C’ wa Kanisa, ambapo pamoja na mambo mengine, Baba Mtakatifu alisema, “Bikira Maria ambaye baada ya kupashwa habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mungu, anakwenda kwa haraka kumtembelea binamu yake Elizabeti, ambaye katika uzee wake, alikuwa ni mjamzito.”
Aidha, aliwaalika Waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kusimama kidete kulinda na kutetea zawadi ya uhai tangu pale mtoto anapotungwa mimba, hadi mauti ya kawaida yanapomfika, kadri ya mpango wa Mungu.
Sambamba na hayo, Baba Mtakatifu anakaza kusema kwamba Kanisa linataka kujitosa kuwahudumia kwa ukarimu na upendo watoto wadogo ambao bado hawajazaliwa zaidi ya wengine wote, kwani hao ni watu wasio na ulinzi wala hatia.
“Wanawake hawa walikuwa na kila sababu ya kufurahia kutokana na miujiza iliyotendwa ndani mwao, mwaliko ni tafakari ya kina kuhusu uwepo wa Mungu kati ya waja wake na kwamba, huruma na upendo wake unamwandama mwanadamu kwa njia ya zawadi ya maisha, kwa kila mtoto anayebebwa tumboni mwa mama yake, kama ilivyo kwa wanawake wengi na kati yao kuna wale ambao wanatazamia kwa imani na matumaini, kuzaliwa kwa watoto wao,” alisema Baba Mtakatifu.
Vile vile, aliwaalika Waamini kupokea zawadi ya uhai kwa moyo wa upendo, shukrani na ukarimu, akisema, “Hata watoto ambao hawajazaliwa, wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Jamii isipojifunza kuwalinda na kuwatunza watu dhaifu, sheria ya mwenye nguvu mpishe, itatawala Dunia. Maskini wanao upendeleo wa pekee mbele ya Mwenyezi Mungu. Wao ni walengwa wa kwanza wa Habari Njema ya Wokovu, ni amana na utajiri wa Kanisa. Wao ni dira na ufunguo wa kuingilia mbinguni.”
Alisema pia kuwa inasikitisha kuona kwamba katika baadhi ya Nchi, utamaduni wa kifo unalindwa kisheria, jambo linalokwenda kinyume cha haki msingi za binadamu, utu na heshima yake.
Aliongeza kwamba maisha ya binadamu ni Matakatifu, hivyo yanapaswa kulindwa na kuendelezwa, akisema kuwa utoaji mimba si kitendo cha maendeleo, bali ni ukiukwaji wa haki msingi za binadamu.
Pia, alibainisha kwamba Kanisa linapenda kuwasaidia wanawake kutekeleza vyema dhamana na wajibu wao wa kulea na kutunza vyema watoto, ambao ni zawadi kubwa kutoka kwa Mungu.
Alisema kuwa katika kipindi hiki cha Sherehe za Noeli ambapo sehemu mbalimbali zinapambwa kwa taa na muziki wa Noeli, Waamini na watu wote wenye mapenzi mema, wanapaswa kuonesha furaha pale wanapokutana na wanawake wajawazito, au wale wanaowabeba watoto wao, tayari kumwimbia Mungu utenzi wa sifa na shukrani, kama ilivyokuwa kwa Elizabeti, akisema “Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na mzao wa tumbo lako amebarikiwa.”
Alisisitiza kwamba hii inatakiwa iwe ni fursa ya kushukuru na kuwabariki watoto wote wanaozaliwa sehemu mbalimbali duniani.

VATICAN CITY

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Taleb Al Abdulmohsen, mwenye umri wa miaka 50, Daktari wa Afya ya Akili, aliyeingia nchini Ujerumani kunako mwaka 2006, hivi karibuni amevamia Soko la Noeli, lililoko mjini Magdeburg, nchini Ujerumani, na kusababisha vifo vya watu watano, na kujeruhi watu zaidi ya 200, na kati yao, watu 41 wako katika hali mbaya.
Kufuatia tukio hilo, Baba Mtakatifu Fransisko amesikitishwa na shambulizi hilo la kinyama, huku akionesha uwepo wake wa karibu kwa waathirika.
Alisema kwamba kwa masikitiko makubwa, anaungana na watu wenye mapenzi mema kuwaombolezea wale wote waliopoteza maisha kutokana na shambulio hilo, na kwamba, yuko karibu na wote walioguswa na kutikiswa na msiba kutokana na tukio hilo.
Aidha, Baba Mtakatifu Fransisko katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, aliwapongeza wale wote wanaoendelea kujisadaka kwa ajili ya kuwahudumia waathirika wa shambulio hilo.
Papa anasali pia na kuwaweka waathirika wote chini ya Kristo Yesu, tumaini la waja wake, nuru inayoangaza kwenye giza la uvuli wa mauti, akiwaombea kwa moyo wote msaada na faraja kutoka mbinguni.
Mji wa Magdeburg ni maarufu sana kwa viwanda na bandari, na upo katikati ya Ujerumani kwenye ukingo wa Mto Elbe, ambapo wachunguzi wa mambo wanasema Taleb Al Abdulmohsen amevamia Soko la Noeli kwa kutoridhishwa na jinsi ambavyo Serikali ya Ujerumani inavyowatendea wakimbizi na wahamiaji, ila yeye bado anashikiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa uchunguzi zaidi.

DODOMA

Na Angela Kibwana

Watu wenye ulemavu sawa na makundi mengine katika jamii, wana haki ya kunufaika na upatikanaji  wa haki ya Afya  ya Uzazi, kama haki ya msingi ya binadamu bila vikwazo, unyanyapaa  na ubaguzi wa aina yoyote.
Haki ya Afya ya Uzazi kwa watu wenye ulemavu imetamkwa na kuelekezwa kwenye Sera, Miongozo na Sheria mbalimbali za Kimataifa, Kikanda na Kitaifa kama vile: Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (2006), kifungu cha 25 (Article 25), umesisitiza watu wenye ulemavu, wana haki ya kupata huduma za afya bila ubaguzi
Sheria ya Tanzania kwa Watu Wenye Ulemavu (2010) kifungu cha 26, Kifungu kidogo cha Kwanza hadi cha tatu limesisitiza kuhusu haki ya kupata huduma ya afya na utengamao kwa watu wenye ulemavu, bila ubaguzi,Sera ya Watu Wenye Ulemavu ya Mwaka 2004, imetambua suala la ulemavu kama haki za msingi za  binadamu.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, imeeleza watu wenye ulemavu ni wale wote wenye changamoto za muda mrefu za kimaumbile, kiakili na katika mfumo wa fahamu (intellectual or sensory), hivyo kukosa na kushindwa kushiriki sawa na makundi mengine ya kijamii katika kuzifikia fursa mbalimbali.
Takribani asilimia 11 ya watu kuanzia umri wa miaka saba (7) na kuendelea, wanaishi na ulemavu wa aina fulani, ikiwa ni ongezeko kutoka asilimia 9.3 (Sensa Mwaka 2012).
Hata hivyo, takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watu wenye ulemavu inatofautiana kati ya kijijini kwa asilimia 11.5 na mjini asilimia 10.6.
Mkoa wa Dodoma una idadi ya watu 299,689, sawa na asilimia 12.3 zaidi ya kiwango cha kitaifa cha asilimia 11, ukiwa ni mkoa wa sita kwa idadi kubwa ya watu wenye ulemavu (Sensa Mwaka 2022) nchini.
Pamoja na jitahada zote zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika na serikali, asasi zisizo za kiserikali na wadau wa maendeleo, kundi la watu wenye ulemavu, wameendelea kukabiliwa na changamoto nyingi za afya ya uzazi, zikijumuisha changamoto za kimazingira na kisera zinazo athiri upatikanaji na ufikikaji wa huduma za Afya, kwa mfano miundo mbinu isiyo rafiki, umbali na gharama za huduma na kukosekana kwa teknolojia saidizi.
Pia, unyanyapaa na mtazamo hasi kutoka kwa wana familia, jamii na watoa huduma za afya dhidi ya  haki ya huduma za Afya ya Uzazi kwa watu wenye ulemavu; Ujumuishaji hafifu wa watu wenye ulemavu kwenye programu na mipango mbalimbali ya afya; watoa huduma za afya kutokuwa na uelewa kuhusu masuala yanayohusu mahitaji ya watu wenye ulemavu, kama vile lugha ya alama, pamoja na namna ya kutoa huduma rafiki kwao; matumizi hafifu, pamoja na kutokuwa na takwimu sahihi za watu wenye ulemavu ili kujumuishwa kwenye mipango, bajeti na huduma za afya katika ngazi ya halmashauri, vituo vya kutolea huduma za afya, na jamii kwa ujumla.
Changamoto hizo zimeongeza uhatarishi zaidi kwa makundi ya wanawake na vijanawenye ulemavu, hali ikiwa mbaya  zaidi kwa wale wanaoishi vijijini wakikabiliwa na umaskini uliokithiri, pamoja na  ukatili wa kingono, kama vile Ubakaji na ndoa za kulazimishwa.
Kwa kutambua changamoto na umuhimu wa haki ya hudumu za Afya ya uzazi kwa watu wenye ulemavu kama ilivyoainishwa katika Sera, Miongozo na Sheria za Kimataifa, Kikanda na Kitaifa; Shirika la Marie Stopes Tanzania, kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Watanzania chini, ya ufadhili wa Marie Stopes International (MSI) kupitia mradi wa Investiment Fund (IF), wameligeukia kundi hili ambalo halijafikiwa ipasavyo  kwa kuwekeza fedha, utaalam na miundombinu, ili kutengeneza mazingira wezeshi kwa watu wenye ulemavu kuzifikia huduma bora za Afya ya Uzazi.
Hayo ni kama vile, Uzazi wa Mpango, Huduma wakati wa Ujauazito, Kujifungua, baada ya kujifungua, Ukatili wa Kijinsia na Ukatili dhidi ya watoto, elimu na taarifa sahihi kuhusu  Afya ya Uzazi na Ujinsia, pamoja na ushiriki wa watu wenye ulemavu katika masuala yanayo athiri maisha yao, ikiwepo Afya Uzazi na Ujinsia kama ilivyoelezwa na Ndugu Goryo Moris Kitege, mtoa huduma za afya ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania
Pia, Ndugu Goryo alisema kuwa Shirika la Marie Stopes Tanzania kwa kushirikiana na Serikali, wanaendelea kuona namna watakavyowajengea uwezo watoa huduma za afya namna kuwahudumia watu wenye ulemavu, pamoja na kufanya ulaghabishi (advocacy), kuhusu uboreshaji wa mazingira wezeshi ili kufikia kundi kubwa la watu wenye ulemavu wa aina mbali mbali nchini.
Kwa mujibu wa  Ndugu  Amina Issa anayeishi na ulemavu wa kusikia kutoka Chama cha Viziwi Dodoma, anasema,  “Mara nyingi hatupati huduma stahiki kutoka kwa watoa huduma za afya kwa kuwa watoa huduma  hawajui Lugha ya Alama”
Pia, Amina anatoa mfano wa unyanyapaa wanaokutana nao watu wenye ulemavu, akisema, “Kuna wakati unakutana na kauli za kudhalilisha, kama vile ‘Hata wewe mtu mwenye ulemavu umeweza kupata ujauzito?’ Kauli hizi zina tuumiza sana,” kwani na sisi tunahisia na tuna haki ya kuwa na familia, pamoja na kufurahia maisha ya mahusiano na ujinsia kama watu wengine” hali hii inakatisha tamaa kwenda kupata huduma.
Vile vile katika kuendeleza jitahada za kuwafikia watu wenye ulemavu katika masuala ya Afya Uzazi; Marie Stopes Tanzania kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA), wameendelea kutoa elimu na huduma bora za Afya ya Uzazi ambapo watu zaidi ya 300 wenye ulemavuwamepatiwa huduma na elimu kuhusu afya ya uzazi.
Justus Ngwantalima, Katibu wa SHIVYAWATA, anasisitiza kwamba ni muhimu kwa jamii kuwa na mtazamo chanya dhidi ya watu wenye ulemavu, ili kufanikisha lengo la usawa katika jamii kwa mujibu wa sera na sheria za nchi.
Kwa mujibu wa Omary Lubuva,  Mwenyekiti wa SHIVYAWATA  Dodoma,kuna haja ya kuboresha mfumo wa mawasiliano ili kuimarisha upatikanaji wa huduma bora  kwa watu wenye ulemavu.
Pia, wataalamu wa afya wanapaswa kupewa mafunzo maalum ya kushughulikia mahitaji ya kundi hili.
Aidha, watu wenye ulemavu wanapaswa kushirikishwa katika kupanga, kutekeleza na kutathmini mipango na bajeti za afya kama ilivyoelekezwa kwenye sera na miongozo mbalimbali ya kimataifa, na ya nchi kwa ujumla.
Hata hivyo, aliwashukuru Marie Stopes Tanzania pamoja na serikali kwa jitahada zao katika kuwashirikisha kushughulikia mahitaji yao; kwani si jambo jepesi kulifikia kundi kubwa kama hili la watu wenye mahitaji maalumu kwa wakati mmoja, hivyo nguvu ielekezwe  pia  kwa watu wenye ulemavu  walio vijijini kwa njia shirikishi na  endelevu.
Katika mahojiano ya mwandishi wetu na Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto wa Wilaya ya Bahi, Ndugu Agnes Mwabungulu, anasema kuwa vituo vingi vya afya havina miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu.
Pia, anabainisha ukosefu wa wataalamu wenye ujuzi wa Lugha ya Alama kama changamoto kubwa.
Hata hivyo, amesema kuwa serikali kwa kutumia rasilimali chache zilizopo, pamoja na kupitia ushirikiano na wadau, wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali zinazo athiri utoaji, upatikanaji na utumiaji wa huduma za afya uzazi kwa watu wenye ulemavu, kulingana na sera na miongozo ya nchi.
Aliongeza kwa kusema  kuwa jitahada za kuwafikia watu wenye ulemavu, hazilengi tu kuwafikia katika hali yao ya uhitaji, bali kuzuia ulemavu kwa watoto wanaowazaa, unaoweza kuchangiwa na kukosekana kwa huduma bora kabla, wakati wa ujauzito, kujifungua na baada ya kujifungua. Hivyo kuongeza changamoto zaidi kwao, serikali, jamii na watoto watakaozaliwa na ulemavu wa aina mbalimbali.
Mwisho, amewashukuru Marie  Stopes Tanzania na wadau wa maendeleo kwa ushirikiano wa, na kazi nzuri wanayoifanya katika Halmashauri ya Bahi, ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za Afya ya Uzazi kwa mtoto na vijana.
Pia, wanawakaribisha kwa ushirikiano zaidi pamoja na wadau wengine, ili kuwakufikia watu wenye ulemavu, pamoja na makundi mengine yenye changamoto katika jamii.

DAR ES SALAAM

Na Remigius Mmavele

Daniel Zitani Ya Ntesa, maarufu kama Ntesa Dalienst, alikuwa mwimbaji\mtunzi wa Kongo ambaye alistawi zaidi katika miaka ya 1970 na 1980.
Anajulikana zaidi kama mmoja wa waimbaji wakuu wa bendi ya TP OK Jazz ya Kongo ambayo ilikuwa bendi maarufu zaidi barani Afrika katika miaka ya 1980.
Alizaliwa Oktoba 30, 1946 huko Kinsiona, Bas Congo. Vipaji vyake vya muziki vilianza kujitokeza pale alipojiunga na kwaya ya shule hiyo, na kuigiza peke yake nyimbo mbalimbali za kwaya hiyo. Baada ya kumaliza shule kuwa mwalimu, akifundisha katika mzunguko wa d’Orientation (CO). Baada ya kufundisha kwa mwaka mmoja, aliondoka na kuendelea na kazi ya muziki.
Mnamo mwaka wa 1966, alijipa Dalienst ya sobriquet, mchezo wa jina lake la Kikristo, na jina lake la mwisho. Mnamo 1967 alijiunga na Vox Africa ambayo ilikuwa mojawapo ya bendi za juu nchini, Zaire wakati huo, ikiongozwa na Jeannot Bombenga.
Na mwaka 1968 alijiunga na bendi ya Festival Des Maquisards iliyokuwa ikiongozwa na Sam Mangwana, ambaye hivi karibuni alikuwa ametoka katika bendi ya Tabu Ley Africa Fiesta National, Maquisards wakati huo ilikuwa moja ya bendi maarufu nchini Zaire na ilikuwa na vipaji vya aina yake Sam Mangwana, Mavatiku Michelino, Dizzy Madjeku. , Jerry Dialungana, Lokombe Ntal na Kiese Diambu ambaye alikuwa binamu wa Dalienst. Washiriki wote wa bendi walijizolea umaarufu mkubwa na TP OK Jazz.
Mnamo 1969, Maquisards waligawanyika na Mangwana kuondoka na kuunda kikundi chake, Dalienst na Dizzy walifikiria kujiunga tena na Vox Africa. Baadaye waliamua kumkaribia Verkys Kiamanguana kwa usaidizi wa Verkys, Maquisards ilifufuliwa kutoka kwenye kitanda chake cha kifo, Wanakuwa moja ya bendi kubwa nchini Kongo inayotoa albamu kadhaa kali kama vile Maria Mboka, Obotama Mobali na Tokosenga na Nzambe nyimbo zote zilizovuma. kutoka kwa Dalienst. Bendi hiyo ilikuwa sasa kama Grand Maquisards.
Miaka ya mapema ya 1970 ilikuwa miaka ya mafanikio makubwa kwa Maquisards huku kukiwa na vibao kama vile Mabala ya Kinshasa na Kaka po na ye ya Dizzy Mandjeku. Sonia ya Diana, Kayumba Martha, na Tolimbisana ya Lokombe, Jarrya na Kiesse Diambu, Mavata, Beneda na Sisi moke ya Dalienst
Kufikia 1974, bendi ilianza kuvunjika kwa sababu ya kutokukubaliana na Verkys. Walikaa mwaka mzima bila kutumbuiza au kuachia nyimbo zozote, na hatimaye bendi hiyo ikaporomoka mwaka wa 1975.
Alijiunga na TP OK Jazz mnamo Septemba 1978 kufuatia kuanguka kwa Macquisards pamoja na Jerry Dialungana. Ilichukua ushawishi mkubwa kutoka kwa Franco kumfanya Dalienst ajiunge, na alipoondoka OK Jazz miezi miwili baadaye, Franco bado alimshawishi kurudi.
Dalients alikuwa wimbo wa papo hapo katika TP OK Jazz, utunzi wake wa mwanzo mwishoni mwa miaka ya 1970 ulijumuisha nyimbo kama vile Tala Ye Na Miso (Mtazame kwa macho), Zaina Mopaya (Zaina the stranger) na Lisolo na Adamo na Nzambe (Mazungumzo ya Adam. na Mungu).
Katika wimbo huo, Dalienst alikumbuka jinsi tangu mwanzo wa wakati, wanaume huwalaumu wanawake kila wakati kwa shida zao wakati kwa kweli wanaume ndio wenye makosa. Wimbo huo haukupokelewa vyema na Makasisi wa Zaire ambao waliuona wimbo huo kuwa unashambulia dini yao. Wimbo huo ulikuwa wa kwanza kati ya nyingi zilizomletea Dalienst sifa ya kuwa mtetezi wa wanawake.
Wakati wanachama 10 wa TP OK Jazz walipokamatwa mwaka wa 1978 na kupelekwa katika gereza maarufu la Makala, Dalienst alikuwa mmoja wa washiriki wachache wa bendi hiyo waliotoroka kukamatwa. Alifaulu kumsadikisha mchungaji huyo kwamba hakuimba nyimbo zozote chafu zilizosababisha kukamatwa.
1980 ilishuhudia wimbo wa kwanza wa Dalienst ‘mega hits’ katika wimbo Liyanzi Ekoti Ngai Motema (Tick imeingia moyoni mwangu), wimbo huo ulijulikana kwa jina la Mouzi.