Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Waaswa kufuata nyayo za Mt.Theresa

Mratibu wa Matikio ya Kanisa wa Tumaini Media, Gaudence Hyera, akimkabidhi Sista Carmela wa Kituo cha Furaha na Amani kiasi cha fedha kilichotolewa na Tumaini Media wakati wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Redio Tumaini ili kusaidia Kituo hicho kilichopo katika Parokia ya Familia Takatifu, Mburahati, jijini Dar es Salaam. Mratibu wa Matikio ya Kanisa wa Tumaini Media, Gaudence Hyera, akimkabidhi Sista Carmela wa Kituo cha Furaha na Amani kiasi cha fedha kilichotolewa na Tumaini Media wakati wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Redio Tumaini ili kusaidia Kituo hicho kilichopo katika Parokia ya Familia Takatifu, Mburahati, jijini Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Wakristo wametakiwa kufuata nyayo za Mtakatifu Theresa wa Kalkuta za kuwasaidia watu wenye uhitaji, hasa wanaoteseka kiroho, ili wawapatie faraja katika maisha yao ya kila siku.
Hayo yalisemwa na Sista Carmela anayefanya utume wake katika Kituo cha Furaha na Amani kilichopo Parokia ya Familia Takatifu – Mburahati, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, baada ya Tumaini Media kufanya matendo ya huruma Kituoni hapo.
“Karibuni katika Kituo hiki cha Furaha na Amani, kama mnavyoona hapa kuna watoto, wazee pamoja na walemavu... Kituo hiki siyo kipya sana, kwani kilianzishwa mwaka 1976, na kimetoa huduma kwa miaka hiyo yote, na bado kinaendelea kutoa huduma.
“Tunafuata nyayo za Mama Theresa wa Kalkuta, kile alichokifanya, na anatamani na sisi tuendelee kukifanya, kuwatembelea na kuwajua wenye shida au wahitaji, siyo tu kwa ajili ya mavazi au chakula, wapo watu wengine ambao wanateseka kiroho, kwa hiyo tunatakiwa kuwagusa waliokata tamaa ili warudi kwa Mungu,” alisema Sista Carmela.
Aliongeza kuwa ni vyema kila mmoja akajitahidi kuwa mwanga kwa wengine, ili wanapomwona yeye, wamwone Mungu kutokena na jinsi yeye anavyoishi.
Sista Carmela aliwashukuru wafanyakazi wa Tumaini Media pamoja na wadau mbalimbali kwa majitoleo yao katika kituo hicho, akiwaomba kuendelea na moyo huo, kwani Mungu anawaita wote ili wawe Watakatifu.
Kwa upande wake, Paroko wa Parokia ya Familia Takatifu- Mburahati, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Vitalis Kassembo aliwashukuru Wanatumaini Media waliokwenda kufanya matendo ya huruma.
“Lakini kwa namna ya pekee tunaishukuru sana familia ya Tumaini Media kwa majitoleo yenu mazuri. Hapa tunajifunza jambo moja - ‘furaha katika kutoa’. Tunapomtolea Mungu, tunabarikiwa zaidi;
“Kwa hiyo Mungu azidi kuwabariki, na hasa Wanatumaini Media tunapomshukuru Mungu kwa miaka 30 ya Utume wetu katika Kanisa, ni miaka mingi sana hiyo. Katika miaka yote hiyo, kuna watu wengi wamefaidika, kuna watu wengi wamepata uponyaji,” alisema Padri Kassembo na kuongeza,
“Tunaendelea kuwashukuru na kuwaombea kwa Mungu ili kazi hiyo iendelee zaidi kwa msaada wa Mungu, na kwa msaada wa Waamini ambao wanaendelea kujitolea kwa hali na mali ili kuhakikisha Injili inamfikia kila mmoja wetu,” alisema Padri Kassembo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Tumaini Media, Arnold Kimanganu alisema kuwa kama Wakristo Wakatoliki, jukumu lao ni kushirikiana, akiongeza kuwa amefarijika kuona namna huduma inavyotolewa katika Kituo hicho.
Kimanganu alimshukuru Padri Kassembo kwa kuwa kiunganishi kizuri kwa Tumaini Media na Kituo cha Furaha na Amani.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.