BERLIN, Ujerumani
Baba Mtakatifu Fransisko ametuma salam zake katika Mkutano wa Kimataifa wa Sala ya Amani wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, huko Berlin, Ujerumani, akisema kuwa vita bado vinaendelea kuitesa dunia.
Katika salamu zake hizo Baba Mtakatifu alisema, “Hatuwezi kujikabidhi…inahitaji kufanya kitu zaidi, inahitaji shauku ya amani ambayo iko kwenye kitovu cha mkutano wenu.”
Alisema kuwa bado haitoshi kuona mazingatio ya kisiasa kwani vipengele vya kimkakati vinavyotekelezwa hadi sasa havijaleta matokeo chanya katika kuleta utulivu duniani.
Baba Mtakatifu Fransisko katika ujumbe huo, aliwaeleza kuwa wanakusanyika pamoja mjini Berlin katika Mlango wa Brandeburg, ambako Wakuu wa Makanisa na Viongozi wa Dini za kidunia, na Mamlaka ya kiraia walioalikwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ambao kwa uaminifu wanaendelea na hija ya sala na mazungumzo yaliyoanzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II huko Assisi, mwaka 1986.
Eneo wanalofanyia mkutano kwa namna ya pekee, linakumbusha hasa jambo la kihistoria; kuanguka kwa ukuta ambao ulikuwa unatengenisha Ujerumani mbili, ukuta huo ulikuwa unagawanya hata dunia mbili za Mashariki na Magharibi mwa Ulaya.
Kuanguka kwake ukuta huo, kulitokana na mchakato wa matukio mbali mbali, ujasiri wa wengi na sala za wengi, zilizofungua njia mpya za uhuru kwa ajili ya watu, kuunganisha familia lakini hata matumaini ya amani mpya ya ulimwengu, baada ya vita vya baridi.
Baba Mtakatifu Fransisko alisema kuwa kwa bahati mbaya kadri miaka inavyokwenda, hapakujengeka matumaini haya ya pamoja, lakini juu ya mafao maalum na juu ya kutokuaminiana kwa mtazamo wa wengine. Kwa njia hiyo, badala ya kuvunja kuta, zimesimikwa nyingine.
Na kuanza kutengeneza mitaro ambayo kwa bahati mbaya na mara nyingi ni fupi. Leo hii vita vimetapakaa sana katika sehemu mbali mbali za dunia. Papa amekumbuka sehemu za Afrika na Nchi za Mashariki ya Kati, lakini pia hata katika kanda nyingi za sayari; na Ulaya, ambayo inafahamika kwa vita vya kwa mgogoro wa Ukraine usiosemekana ambao hauoni mwisho, na umesababisha vifo, majeruhi, uchungi, kuhama na uharibifu.
“Mwaka jana nilikuwa nanyi huko Roma, katikka uwanja wa Masalia ya Kale (Koloseo), kuombea amani.”